Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2025

DCEA YATOA ELIMU KWA WALIMU WAKUU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ZA JIJI LA ARUSHA

Picha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 25.02.2025 imetoa elimu juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya kwa walimu wakuu zaidi ya 200 wa Shule za Msingi na Sekondari za Jiji la Arusha katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Kijenge.  Walimu hao walielezewa uhusiano uliopo kati ya tatizo la dawa za kulevya na changamoto ya afya ya akili, kuwa matumizi ya dawa za kulevya huamsha magonjwa ya akili. Pia walikumbushwa wajibu wao kama walimu wakuu wa kusimamia programu mbalimbali za kuondoa tatizo la dawa za kulevya na afya ya akili shuleni kwao.  Walimu hao walisisitizwa kuendelea kushirikiana na Mamlaka kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kupitia namba ya simu ya bure ya 119

SERIKALI YAKOSHWA MAANDALIZI KABAMBE SIKU YA WANAWAKE ARUSHA.

Picha
  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na makundi maalum Dkt. Doroth Gwajima amefika Mkoani Arusha na kukagua maandalizi ya Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, ambayo kitaifa yatafanyika Mkoani Arusha, akiridhishwa na maandalizi mazuri na kutangaza kuwa Kiwango cha maandalizi yanayofanywa Mkoani Arusha kitakuwa kiwango cha kutolewa mfano kwenye maadhimisho yajayo. Waziri Gwajima aliyeambatana na washauri wa Rais Mhe. Sophia Mjema na Mhe. Angellah Kairuki, wakati akizungumza na Kamati za maandalizi ya maadhimisho hayo Jijini Arusha, ameagiza kuandaliwa kwa Kamati ndogo itakayoangazia maandalizi ya maadhimisho hayo ngazi ya Mkoa na kuahidi kutangaza Mikoa iliyofanya vizuri mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, anayetarajiwa kuwa Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo kwa mwaka huu. "Mikoa ipo mingi na mimi nilijiuliza Arusha mmepataje hii fursa, Kumbe ndiyo mambo yenu haya? Arusha hamna jambo dogo, mmefunika kwa maandalizi yenu, wamejiandaa kote ila ninyi ni namba moja. Standar...

RC MAKONDA AMEWAAGIZA MADIWA WA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA WAKAMILISHE MIRADI YOTE

Picha
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewaagiza madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kuhakikisha wanakamilisha miradi yote ya viporo ikiwemo ujenzi wa barabara, soko na stendi ya kisasa. Makonda ameyasema hayo katika kikao cha Baraza Maalum la Madiwani la kupitisha bajeti ya Sh bilioni 119 huku makusanyo ya mapato ya ndani yakiwa ni Sh milioni 51.2 kwa mwaka 2025/2026. “Haiwezekani miradi inapoanza maneno yanakuwa mengi ilhali wananchi wanahitaji maendeleo hakikisheni miradi yote viporo ikamilishwe kwa wakati lakini pia pandeni miti msipande fitna,”amesema Makonda. RC Makonda amesema anataka mkoa huo kuwa namba moja kwa kila kitu na kwamba hawatokubali mkoa huo kupunguza mapato waliyojiwekea bali mapato yaongezeke ikiwemo kila diwani kuhakikisha maendeleo katika kata yake yanakuwa ikiwemo miradi ya maendeleo Wakati huo huo, Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha wamemwomba RC Makonda kuchukua fomu ya kugombea ubunge mwaka 2025 ili kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa ajili ya utatuzi ...

RC MAKONDA AKARIBISHA UWEKEZAJI ZAIDI KUTOKA SHIRIKA LA FAO, UBELGIJI NA SWITZERLAND.

Picha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Jumatatu Februari 24, 2025 amekutana na kuzungumza na Balozi wa Ubelgiji kwenye shirika la Chakula na kilimo duniani FAO Mhe. Levien De La Marche na Balozi wa Switzerland kwenye Umoja wa Mataifa Mhe. Kristztina Bende, ambao wameambatana na Maafisa waandamizi wa shirika hilo la Chakula, wakiwa Mkoani Arusha kutembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika hilo Wilayani Monduli na Karatu. Katika mazungumzo yao pamoja na mambo mengine, Mhe. Makonda amewasilisha maombi yake ya kuwaomba Mabalozi hao kuwa Mabalozi wa kuvutia Uwekezaji Mkoani Arusha kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya matibabu, akiwahakikishia  usalama, Mazingira bora ya uwekezaji pamoja na ushirikiano wa kutosha kutoka kwenye Ofisi yake katika kuhakikisha kuwa uwekezaji wao unakuwa wa manufaa. Mhe. Makonda amewaeleza kuhusu jitihada mbalimbali za kuimarisha ulinzi na usalama kwenye Mkoa wa Arusha tangu kuteuliwa kwake kuongoza Mkoa huo, akisema tamanio la ...

KIKAO CHA KAWAIDA CHA BARAZA LA WAZAZI WILAYA YA ARUSHA

Picha
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Arusha Ally Mwinyimvua,amefungua kikao hicho cha Baraza la wazazi wilayani humu na kuwahasa jumuiya hiyo kuendeleza mshikamano na ushirikiano mkubwa kueleke uchaguzi mkuu 2025 kwa kuwa wamoja na kuyaacha mengine. Pia Ameitaka jumuiya hiyo kuepuka chuki na kuacha kuchukiana wenyewe kwa wenyewee ilikuendelea kukijenga chama kuwa imara zaidi.

SERIKALI YAMSOMEA MASHTAKA 60 YA UHUJUMU UCHUMI NA UTAKATISHANI MFANYABIASHARA ΝΑ MWEKEZAJI MZAWA ARUSHA, YAJIPANGA NA MASHAHIDI 80 NA VIELELEZO 461!

Picha
SERIKALI imemsomea mashtaka 60 ya uhujumu uchumi, mfanyabiashara na mwekezaji Saleh Salimu Alamry (54) Mkazi wa Njiro Jijini Arusha akikabiliwa na mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu, kughushi na utakatishaji fedha haramu kiasi cha dola za kimarekani milioni 8 akiwa mkurugenzi mwenza wa kampuni mbili za uwindaji na utalii ya Sunset Tarangire limited na Alrajhi Holdings LTD Mwingine aliyesomewa mashtaka ni wakili wa kujitengemea Sheck Mfinanga ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo. Akisoma mashtaka hayo leo februari 20,2025 mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha, Erasto Philly, wakili wa serikali mwandamizi, Edgar Batulaki akisaidiana na Jackline Mosha na Alawi Miraji, alisema agosti mwaka jana walipata malalamiko kutoka kwa wabia wenzake Khaled Alrajhi na Abdulkarim Alrajhi raia wa nchi ya Saud Arabia. Wakili alisema kuwa wabia wenzake kupitia kampuni yao ya Sunset Tarangire limited na Alrajhi Holdings LTD walidai kuwa Saleh A...

DCEA KUPITIA OFISI ZA KANDA IMEFANIKIWA KUKAMATA KILOGRAMU 790.528 ZA DAWA YA KULEVYA.

Picha
  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, imeteketeza ekari 336 za mashamba ya bangi yaliyokuwa ndani ya hifadhi ya Ikome wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma yakiwa yamechanganywa na mazao mengine halali ili kuficha shughuli hiyo haramu, Aidha, katika operesheni hiyo, kilo 148 za mirungi zilkamatwa. Akizungumza wilayani Kondoa wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo, leo tarehe 18 Februari, 2024 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo ameeleza kuwa, operesheni hiyo ni hatua kubwa katika vita dhidi ya dawa za kulevya. "Hii ni operesheni kubwa ya kwanza kufanyika mkoani Dodoma, ikionyesha wazi kuwa kilimo cha bangi kimeanza kuenea katika baadhi ya maeneo ya mkoa huu. Tutaendelea kuchukua hatua kali kuhakikisha kuwa uzalishaji, biashara na matumizi ya dawa za kulevya vinadhibitiwa kwa nguvu zote," alisema Lyimo. Pamoja na operesheni hiyo ameongeza kuwa, katika kipin...

MAHIZA AZIONYA NGOs ZINAZOKIUKA MAADILI

Picha
Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini, Mwantumu Mahiza, amesema kumekuwapo na ongezeko la mashirika yanayokiuka maadili kwa kisingizio cha kusaidia jamii. Moshi.Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini, Mwantumu Mahiza, ameyataka mashirika hayo (NGOs) kufanya kazi kwa mujibu wa malengo yao ya usajili na kuacha kuhamasisha ajenda zinazokiuka maadili ya Kitanzania. Mahiza anetoa rai hiyo leo Februari 18,2025 wakati wa mkutano wa viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali uliofanyika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, ambapo amesema kumekuwapo na ongezeko la mashirika yanayokiuka maadili kwa kisingizio cha kusaidia jamii. "Kila shirika lililosajiliwa lifanye kazi kwa mujibu wa lengo lake. Uzoefu umeonyesha kuwa baadhi ya mashirika yamesajiliwa kwa shughuli fulani, lakini utekelezaji wake unaenda kinyume na maadili yetu kwa kuingiza ajenda zisizo sahihi," amesema Mahiza. Amesema Mkoa wa Kilimanjaro umekuwa na changamoto...

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA ARUSHA ATEMBELEA NA KUKAGUA JENGO LA UTAWALA LA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA

Picha
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Mhe. Maxmillian Iranqhe mapema hii leo amefanya ziara ya kushitukiza kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo Jipya la Utawala la Halmashauri ya Jiji la Arusha.  Katika ziara hiyo,Mhe. Mstahiki Meya ametoa pongezi kwa timu nzima ya ujenzi na kusisitiza uwepo wa kasi ya ujenzi ili kufikia malengo. Kwa upande wake Mhandisi Mshauri wa jengo hilo Ndg. Rashid Kapwani amesema kwa sasa hatua iliyofikiwa ni kuondoa Milunda katika sakafu ya kwanza. Mbali na Mhe. Mstahiki Meya,hamasa kubwa imeendelea kutolewa na viongozi mbalimbali wa Jiji akiwemo Mkuu wa Mkoa,Mhe. Paul Makonda,Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Ndg. John L. Kayombo na Waheshimiwa Madiwani wote lengo likiwa ni kuvuka malengo ya kukamilika kwa jengo hilo. Aidha,katika ziara hiyo,Mhe. Mstahiki Meya aliambatana na Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Bi.Deborah Ngangaji. Ujenzi wa Jengo Jipya la Utwala la Halmashauri ya Jiji la Arusha ulianza mnamo tarehe 04/7/2024 ambapo k...

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA APOKELEWA NA RC CHONGOLO SONGWE

Picha
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ndugu *Fadhili Maganya* amewasili katika mkoa wa Songwe rasmi kwa ajili ya kuanza ziara yake na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Daniel Chongoloambaye amemweleza namna ilani ilivyotekelezwa kwa vitendo. Chongolo amesema kuwa ndani ya miaka minne ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan madarakani mkoa umeimarika kimaendeleo na kiuchumi huku akimuahidi zawadi ya kura za ushindi kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu. Baada ya kusaini kitabu cha wageni, Maganya alimshukuru Chongolo kwa mapokezi mazuri aliyompa wakati alipowasili katika ofisi yake.

DCEA, POLISI, WADAU NA WARAIBU DAWA ZA KULEVYA WASHEHEREKEA PAMOJA SIKUKUU YA WAPENDANAO JIJINI ARUSHA

Picha
  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi tarehe 15.02.2025 jijini Arusha imejumuika pamoja na Wadau wa Mamlaka na Waraibu wa dawa za kulevya kusheherekea Sikukuu ya Wapendanao Duniani katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.  Mgeni rasmi katika Sherehe hizo alikuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD) SSP. Georgina Matagi ambapo katika hotuba yake aliiomba jamii kutowanyanyapaa waraibu wa dawa za kulevya na badala yake inatakiwa kuendelea kuwapenda, kuwaheshimu, kuwathamini, kuwajali na kuwawezesha kufikia malengo yao kwani uraibu ni ugonjwa na unatibika. *_Washiriki wa Sherehe hizo zaidi ya 120 walihamasishwa kuendelea kushirikiana na Mamlaka katika mapamabano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa kuendelea kutoa taarifa za wahalifu wa dawa hizo katika maeneo yao wanayoishi kwa kupiga namba ya  bure 119.

VALENTINE DAY YANOGESHWA NA DIKO LA AMBONI TANGA

Picha
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imehitimisha Kampeni ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mapango ya Amboni, Tanga Leo tarehe 14 Februari, 2025 ambapo  wananchi mbalimbali walihamasika kufanya utalii wa ndani katika siku ya wapendanao (Valentine day)  na kufurahia pishi la vyakula vya asili hasa kwa watu wa Tanga. Akizungumza wakati wa kuhitimisha Kampeni ya kuhamaisha utalii wa ndani katika eneo la Mapango iliyoambana na mashindano ya Mapishi, Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mh. Japhari Kubecha ameupongeza uongozi wa NCAA kwa Ubunifu ambapo kupitia kampeni imeongeza  hamasa kubwa ya utalii wa ndani katika mkoa wa Tanga. "Niendelee kuipongeza NCAA kwa ubuhifu wao mkubwa wa kukuza utalii ndani ya Mapango ya Amboni. Niwaahidi kwamba serikali ya Wilaya ya Tanga itaendelea kushirikiana na nyie kuendeleza na kutunza mapango haya ya pekee" Alisema Mhe. Kubecha Kwa upande wake Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia huduma za utalii na Masoko NCAA, Mariam Kobelo ...