MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA ARUSHA ATEMBELEA NA KUKAGUA JENGO LA UTAWALA LA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Mhe. Maxmillian Iranqhe mapema hii leo amefanya ziara ya kushitukiza kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo Jipya la Utawala la Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Katika ziara hiyo,Mhe. Mstahiki Meya ametoa pongezi kwa timu nzima ya ujenzi na kusisitiza uwepo wa kasi ya ujenzi ili kufikia malengo.
Kwa upande wake Mhandisi Mshauri wa jengo hilo Ndg. Rashid Kapwani amesema kwa sasa hatua iliyofikiwa ni kuondoa Milunda katika sakafu ya kwanza.
Mbali na Mhe. Mstahiki Meya,hamasa kubwa imeendelea kutolewa na viongozi mbalimbali wa Jiji akiwemo Mkuu wa Mkoa,Mhe. Paul Makonda,Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Ndg. John L. Kayombo na Waheshimiwa Madiwani wote lengo likiwa ni kuvuka malengo ya kukamilika kwa jengo hilo.
Aidha,katika ziara hiyo,Mhe. Mstahiki Meya aliambatana na Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Bi.Deborah Ngangaji.
Ujenzi wa Jengo Jipya la Utwala la Halmashauri ya Jiji la Arusha ulianza mnamo tarehe 04/7/2024 ambapo kwa sasa umefikia 44% unatarajiwa kukamilika kwa awamu ya kwanza ifikapo tarehe 03/7/2025.




Maoni
Chapisha Maoni