Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2024

BILIONEA MULOKOZI APEWA TUZO NA CHUO CHA KIJESHI CHA UKAMANDA NA UNADHIMU (CSC)

Picha
  Kampuni ya Mati Super Brands Limited inayozalisha vinywaji changamshi yenye makao yake Makuu Mjini Babati Mkoani Manyara imepewa tuzo ya maalumu kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kusaidia jamii inayowazunguka Pamoja na kushirikiana na taasisi mbali mbali za kiserikali. Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) chenye makao yake Mkoani Arusha , Colonel Verus Chrysostom Mbuzi katika ziara maalumu ya kimafunzo iyofanywa na Maafisa hao wa ngazi za juu wa Kijeshi kutoka mataifa mbali mbali katika kampuni ya Mati Super Brands Ltd.  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi ametoa shukrani zake kwa Chuo hicho cha kijeshi kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika masuala mbali mbali ikiwemo kurudisha sehemu ya faida wanayoipata kwa jamii inayowazunguka. Mulokozi amesema kuwa Tuzo hiyo inawapa chachu ya kuendelea kufanya vizur...

EWURA YARAHISISHA UJENZI WA VITUO VYA MAFUTA VYA GHARAMA NAFUU MAENEO YA PEMBEZONI NA VIJIJINI ,GHARAMA ZA MAOMBI YA UJENZI NI SAWA NA BUR

Picha
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),imekuja na mpango wezeshi kwa wafanyabiashara kuwekeza vituo vya mafuta kwa gharama nafuu katika maeneo ya pembazoni na vijijini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo na kuondoa hatari ya kuuza mafuta kiholela. Akiongea na vyombo vya Habari katika viwanja vya maonesho ya nanenane Njiro, Arusha, Meneja wa EWURA kanda ya Kaskazini, Lorivii Long'idu alisema EWURA imewataka wafanyabiashara kujenga vituo vya mafuta kwa gharama nafuu na kwa njia salama ili kuwarahisishia wamiliki wa vyombo vya moto wakiwemo bodaboda kupata huduma hiyo kwa njia salama isiyo hatarishi. "Tupo hapa katika maonesho ya Nanenane kutoa elimu kwa umma juu ya utaratibu wetu mpya wa kuwezesha wafanyabiashara kutoa huduma ya mafuta kwa njia salama kwa kurahisisha utoaji wa vibali vya ujenzi katika maeneo ya pembezoni na vijijini " Alisema kumekuwepo na utaratibu wa uuzaji wa mafuta kwa njia ya chupa na madumu unaotokana na ongezezo la uhitaji ...