Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2025

JK ASHIRIKI KUTOA MAFUNZO CHUO KIKUU CHA HAVARD HUKO BOSTON KWA MAWAZIRI WA NCHI ZINAZOENDELEA

Picha
Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete yuko mjini Boston, Marekani, ambako anashiriki katika kutoa mafunzo kwa Mawaziri wa Fedha na Mawaziri wa Mipango kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea.  Mafunzo hayo yanafanyika chini ya Mpango wa Uongozi wa Ngazi ya Mawaziri wa Harvard, maarufu kama Harvard Ministerial Leadership Program, unaoendeshwa na Chuo Kikuu cha Harvard. Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Kikwete ni mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu walioalikwa kushiriki kama wakufunzi, wakitumia uzoefu wao wa uongozi kuhamasisha na kuwajengea uwezo viongozi wa kizazi kipya. Mbali na Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu, mafunzo haya pia yanashirikisha Wakuu wa Taasisi za Kimataifa, wawakilishi wa mashirika binafsi, pamoja na mabingwa wa masuala ya sera, uchumi na maendeleo kutoka maeneo mbalimbali duniani.

JUKWAA LA KIMATAIFA LA UTALII WA VYAKULA KUKUTANISHA WABOBEZI WA UTALII ZAIDI YA 300

Picha
Jukwaa la Pili la Kimataifa la Utalii Wa Vyakula la Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) Kanda ya Afrika lililoanza leo Aprili 22, 2025 jijini Arusha linatarajia kukutanisha washiriki takribani 300 wakijumuisha viongozi waandamizi katika sekta ya utalii na ukarimu, watumishi wa serikali, pamoja na wataalamu wa masuala ya upishi kutoka ndani na nje ya Afrika. Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Hoteli ya Gran Melia jijini Arusha. “Tukio hili linalenga kuangazia uhusiano muhimu kati ya utamaduni wa upishi na utalii, pamoja na kufanya tathmini ya mchango wa utalii wa vyakula katika kukuza maendeleo ya kiuchumi, kuhifadhi urithi wa kiutamaduni, na kuboresha maisha ya jamii linaandaliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism), pamoja na Basque Culinary Center” amesema Mhe. Chana. Amefaf...

KUELEKEA PASAKA; DCEA NA MAADILI KANDA YA KASKAZINI WAFANYA MATENDO YA HURUMA KWA WARAIBU ARUSHA

Picha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini tarehe 16.04.2025 imetoa msaada wa vifaa mbalimbali katika Nyumba Mbili za Upataji Nafuu zinazokaliwa na Wanaume na Wanawake zilizopo Olmotonyi na Moshono jijini Arusha.  Lengo la kutoa msaada huo kwa waraibu hao ni kuonesha kuwathamini, kuwajali, kuwapenda na kuwatia moyo waraibu wanaoendelea kupata nafuu katika nyumba hizo pamoja na kuwaonesha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ipo pamoja nao katika mchakato wa kupona uraibu wa dawa za kulevya. *_Aidha, Ofisi za DCEA na MAADILI Kanda ya Kaskazini zimetoa wito kwa wananchi kuendelea kukuza maadili yaliyokuwa mema katika jamii sababu maadili mabaya ndo sababu ya maovu yote katika jamii ikiwepo kujihusisha na matumizi au biashara haramu ya dawa za kulevya._* *_MWISHO_*

JK AWAILISHA SALAMU ZA RAIS SAMIA KWA KEPTENI IBRAHIM TRAORE, KIONGOZI WA KIJESHI WA BURKINA FASO MJINI OUAGADOUGOU LEO

Picha
Rais Mstsaafu wa Awamu ya Nne na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kiongozi wa Burkina Faso Kepteni Ibrahim Traore mjini Ouagadougou na kushuhudiwa na baadhi ya maafisa waandamizi wa nchi zote mbili. Mhe. Kikwete aliwasilisha pia salamu za Rais Samia ambazo zilielezea umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kijamii na kiuchumi kama njia muhimu kwa bara hilo kujitegemea, hususan katika kipindi hiki ambapo misaada kutoka nchi za magharibi imepungua kwa kiasi kikubwa.

DCEA KANDA YA KASKAZINI YATEKETEZA KILOGRAMU 94.828 ZA DAWA YA KULEVYA AINA YA MIRUNGI

Picha
OFISI YA MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA KANDA YA KASKAZINI KWA NIABA YA KAMISHNA JENERALI WA DCEA  ARETAS  LYIMO LEO TAREHE 09.04.2025 IMETEKETEZA KIASI CHA KILOGRAMU 94.828 CHA DAWA ZA KULEVYA AINA MIRUNGI KATIKA DAMPO LA H/SHAURI  LILILOPO ENEO LA MAJI YA CHAI WILAYANI ARUMERU. UTEKETEZAJI VIELELEZO HIVI UMEHUSISHA WADAU WOTE MUHIMU KWA MUJIBU WA TAKWA LA KISHERIA. UTEKETEZAJI WA VIELELEZO HIVYO NI MATOKEO YA MAFANIKIO YA OPERESHENI YA UKAMATAJI WA WATUHUMIWA WA BIASHARA NA WASAFIRISHAJI WA DAWA ZA KULEVYA AINA YA MIRUNGI  ILIYOFANYIKA TAREHE 04.04.2025 KATIKA MAENEO YA KIJENGE KUSINI KATA YA KIMANDORU MKOANI ARUSHA AMBAPO JUMLA YA WATUHUMIWA SITA WALIKAMATWA KWA MAKOSA YA KUHUSIKA NA UHALIFU HUO. MAMLAKA INATOA RAI KWA WANANCHI WANAOISHI KATIKA MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI AMBAYO NI ARUSHA, KILIMANJARO, MANYARA NA TANGA KUTOJIHUSISHA KWA NAMNA YOTOTE NA DAWA ZA KULEVYA KWANI ADHABU YAKE NI HADI KIFUNGO CHA MAISHA JELA. *_MWISHO_*

WAMILIKI NA MAMENEJA KUMBI ZA STAREHE ARUSHA WAPATIWA ELIMU YA MADHARA YA DAWA ZA KULEVYA

Picha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 07.04.2025 jijini Arusha imetoa elimu kinga kwa wamiliki na wasimamizi wa kumbi na sehemu za sterehe na burudani wapatao 18 kuhusu madhara ya dawa za kulevya pamoja na kuwapatia mbinu wanazoweza kutumia katika udhibiti wa matumizi ya dawa za kulevya katika maeneo yao ya kazi wanayoyasimamia. Aidha, Wasimamizi wa maeneo hayo ya starehe  walielezwa hatari na madhara ya kiafya ya kuchanganya Shisha na dawa za kulevya  kuwa adhabu yake ukibainika kutenda kosa hilo ni kifungo cha miaka mitatu na faini isiyopungua shilingi za kitanzania milioni tano au adhabu zote mbili kwa pamoja.  Wamiliki na Mameneja wa Kumbi na maeneo ya Starehe walioshiriki Kikaokazi hicho waliombwa kuwa Mabalozi wa Mamlaka katika kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya katika maeneo yao ya kazi wanayoyasimamia ambapo katika kutilia mkazo suala hilo Ofisi ya Mamlaka Kanda ya Kaskazini iliandaa Mkataba rafiki kati ya Ofisi h...