Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2026

*BALOZI KAGANDA ATEMBELEA OFISI ZA TPA NCHINI ZIMBABWE*

Picha
Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Kamishna wa Polisi (CP) Suzan Kaganda, ametembelea ofisi za Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) zilizopo mjini Harare na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa TPA nchini humo, Bi. Kulthum Boma kuhusu namna ya kuimarisha huduma na kuongeza ufanisi katika usafirishaji wa mizigo kupitia bandari za Tanzania. Ziara ya Mheshimiwa Balozi Kaganda ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Diplomasia ya Uchumi, ikiwa na lengo la kutambua na kuendeleza mchango wa TPA katika usafirishaji wa mizigo kutoka bandari za Tanzania kwenda nchi za Kusini mwa Afrika, ikiwemo Zimbabwe. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Bi. Kulthum Boma alieleza kuwa ofisi hiyo, yenye jukumu la masoko na huduma kwa wateja, imekuwa na mchango chanya katika kuongeza shehena ya mizigo inayoingia Zimbabwe kupitia bandari za Tanzania tangu kufunguliwa kwake rasmi mwaka 2023. Kwa upande wake, Mheshimiwa Balozi Kaganda amepongeza mafanikio hayo na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya ofisi...

KAMANDA MASIJA ATOA WITO DHIDI YA UHALIFU WA KIMTANDAO

Picha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Shadrack Masija, ametoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu wanapotumia mitandao ya mawasiliano na majukwaa ya kidijitali ili kujiepusha na vitendo vya uhalifu wa kimtandao vinavyoendelea kujitokeza katika jamii. Kamanda Masija ametoa wito huo Machi 13, 2026 wakati akishiriki futari (iftar) iliyoandaliwa na mtandao wa simu wa Yas katika Ukumbi wa Country Hotel uliopo Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, hafla iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa mawasiliano na wananchi. Akizungumza katika hafla hiyo, SACP Masija amesema kumekuwa na ongezeko la matukio ya uhalifu wa kimtandao ikiwemo utapeli kupitia simu na mitandao ya kijamii, ambapo baadhi ya watu hutumia teknolojia vibaya kwa lengo la kujipatia fedha au taarifa za wengine kwa njia zisizo halali. Kutokana na hali hiyo, amewahimiza wananchi kuwa makini wanapotumia simu na mitandao ya kijamii kwa kuepuka kutoa taarifa zao binafsi kwa watu wasiofahamika pamoja n...