MSIMAMIZI WA UCHAGUZI ARUSHA MJINI: WALIOPOTEZA KADI YA KURA WATARUHUSIWA KUTUMIA NIDA, LESENI AU PASI YA KUSAFIRI.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Arusha Mjini ametangaza rasmi kuwa Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika siku ya Jumatano, tarehe 29 Oktoba 2025, kwa mujibu wa Kifungu cha 69(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024. Kwa mujibu wa tangazo hilo, vituo vilivyotumika kuandikisha wapiga kura ndivyo vitakavyotumika kupigia kura siku ya uchaguzi. Vituo hivyo vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi (2:00) na kufungwa saa 10:00 jioni (10:00). Aidha, kwa wapiga kura wa magereza, vituo vyao vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi (2:00) na kufungwa saa 9:00 alasiri (9:00). Taarifa Muhimu kwa Wananchi Sambamba na tangazo hilo, kwa kila kituo cha kupigia kura zimebandikwa taarifa zifuatazo: Mfano wa karatasi ya kura yenye majina, picha, na nembo za vyama vya wagombea wa nafasi za Rais, Wabunge na Madiwani; Orodha ya majina ya wapiga kura walioandikishwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi; Orodha ya wapiga kura waliopangiwa kupiga kura ya Rais pekee. Wananchi wote wanahi...