Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2025

*ARUSHA KULIKUWA NA VURUGU NA UPORAJI SI MAANDAMANO- RC MAKALLA*

Picha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amesema kilichofanyika Mkoani Arusha na katika baadhi ya Miji na Majiji ya Tanzania Oktoba 29, 2025 ni vurugu, uporaji na uharibifu na si maandamano. Mhe. Makalla ameyasema hayo leo Novemba 30, 2025 mbele ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kwenye mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya Magufuli, Arumeru, akieleza kuwa katika vurugu hizo, maduka yalivunjwa, bidhaa kuibiwa, uporaji wa fedha pamoja na uchomaji wa Vituo vya kuuza mafuta, magari, Majengo ya Polisi na mahakama za ngazi mbalimbali katika Mkoa wa Arusha na maeneo mengine. Akinukuu kamusi ya Kilatini, Mhe. Makalla amesema Maandamano ni kikundi cha watu wanaotembea pamoja kwa utaratibu maalum na ujumbe maalum, akisema kuwa kamwe Mkoa wa Arusha hautaruhusu vurugu kujitokezs tena na akiwakaribisha Watalii na Taasisi mbalimbali kufika Mkoani Arusha ili kutalii pamoja na kufanya mikutano yao na kuwahakikishia amani na usalama wa kutosha. Awali Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Lameck...

*WAZIRI MKUU AWASILI ARUSHA KWA ZIARA YA SIKU MOJA*

Picha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba leo Jumapili Novemba 30, 2025, amewasili Mkoani Arusha kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wa Serikali, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu. Mhe. Waziri Mkuu anafanya ziara ya Kikazi ya siku moja Mkoani Arusha ambapo pamoja na mambo mengine, anatarajiwa kuwa na Mkutano mkubwa wa hadhara kwenye Viwanja vya Magufuli, Leganga, Kata ya Usa River, Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

BOLT YAZUA GUMZO ARUSHA, AJIRA ZA VIJANA NA WANAWAKE ZAPAA

Picha
Mkutano wa wataalamu wa mawasiliano zaidi ya 100 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umefanyika jijini Arusha na kuibua mijadala mikubwa kuhusu uaminifu kati ya wananchi na taasisi pamoja na nafasi ya sekta binafsi katika kuboresha huduma. Mkutano huo unaojulikana kama East Africa PR Week umehusisha maofisa uhusiano kutoka sekta mbalimbali huku kampuni ya usafiri wa mtandaoni Bolt ikivuta hisia za wengi kutokana na mchango wake katika kuleta ajira na kuchochea uchumi wa Tanzania . Akizungumza kwenye Meneja mahusiano ya umma kampani ya kimataifa ya usafiri bolt Tanzania Gilbert Ginono kutoka Bolt alisema kampuni hiyo imekuwa sehemu muhimu ya mabadiliko ya kiuchumi nchini na imewafungulia vijana wengi milango ya ajira kupitia shughuli za uendeshaji na usafiri wa mtandaoni.  Amesema vijana wengi sasa wanategemea Bolt kupata kipato cha kila siku na kwamba mfumo huo wa kidigitali umeongeza mzunguko wa fedha na kutoa matumaini kwa wanaotafuta ajira mijini. Kinono ames...