TAARIFA ZA TEKNOLOJIA YA MIKANDA YA VISUKUMA MAWIMBI KUKUZA UTALII
Afisa Mhifadhi Mkuu kutoka TANAPA, Davis Mushi amesema zoezi la kuwafunga tembo teknolojia ya mikanda ya visukuma mawimbi mbali na kudhibiti makundi ya tembo yanayoleta changamoto kwa wananchi, taarifa za teknolojia hiyo zitachochea utalii na uhifadhi wa tembo kwa huonesha mienendo ya tembo katika misimu mbalimbali ya mwaka. Mtafiti na daktari wa wanyamappri kutoka TAWIRI Dkt.Mikidadi Mtalika amesema zoezi hilo limelenga kufuatilia zaidi ya tembo mia moja katika Wilaya za Kilombero na Morogoro Vijijini ambapo hadi tarehe 12 Mei, 2026 tembo viongozi wa makundi manne (4) yenye zaidi ya tembo 40 wamefungwa mikanda ya visukuma mawimbi na zoezi linaendelea. Wakati zoezi hilo likiendelea, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Six Rivers Afrika, Bw. Brandon Kempt, akiwa uwandani ametangaza neema kwa TANAPA na TAWIRI “Wanafanya kazi nzuri, sisi kama wadau wa kimataifa hatuna budi kuhamasisha dunia kuthamini urithi wa maliasili iliyopo Tanzania na kutuunga mkono kuziwezesha TANAPA na TAWIRI kutek...