DCEA YAHITIMISHA MAFUNZO YA KIMATAIFA KATIKA KUWAJENGEA UWEZO ASASI ZA KIRAIA JIJINI ARUSHA*
DCEA yazijengea uwezo Asasi za Kiraia Arusha kwa kuwapa miongozo sahihi ya uelimishaji umma ngazi ya familia_* Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Taasisi ya Colombo Plan Drug Advisory Programme (CP-DAP) tarehe 22.05.2025 imehitimisha mafunzo maalum ya siku 5 ya kuwajengea uwezo Asasi za Kiraia juu ya Mtaala wa Kimataifa wa utoaji elimu kinga sahihi dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa ngazi ya familia (Universal Prevention Curriculum-UPC Family Based Prevention) kwa Wawakilishi wa Asasi za Kiraia 24 katika Ukumbi wa YCR uliopo Ngarenaro jijini Arusha. Mafunzo hayo ya siku tano yamewaweza washiriki hao kupata mbinu mpya zilizothibitishwa kisayansi zitakazowasaidia katika kutoa elimu kinga ngazi ya familia. Aidha, washiriki wa mafunzo hayo walipatiwa vyeti vinavyotambulika kimataifa katika utoaji elimu sahihi dhidi ya tatizo la dawa za kulevya. Hivyo, wataalamu hao wataenda kuisaidia jamii ya kitanzania katika k...