Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2025

DCEA YATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA CHAMA CHA WALIMU (CWT) MKOA WA ARUSHA

Picha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 30.01.2025 imetoa elimu juu ya mbinu za kuwaepusha wanafunzi na tatizo la dawa za kulevya kwa viongozi 58 wa matawi ya Chama cha Walimu (CWT) Mkoa wa Arusha katika Ukumbi wa Ofisi za Chama hiko jijini Arusha.  Walimu Viongozi hao walifundishwa uhusiano wa tatizo la dawa za kulevya na changamoto za afya ya akili, kuwa matumizi ya dawa za kulevya kwa wanafunzi inaweza kupelekea kupata magonjwa ya akili na kufeli darasani.  Pia walihamasishwa kushirikiana na Mamlaka katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa hizo kupitia namba ya simu ya bure ya 119.

MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA KANDA YA KASKAZINI IMETEKETEZA KILOGRAMU 204.8165 ZA DAWA ZA KULEVYA JIJINI ARUSHA

Picha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa niaba ya Kamishna Jenerali *ARETAS JAMES LYIMO* leo tarehe 29.01.2025 imeteketeza Kilogramu 204.8165 za dawa za kulevya katika Dampo la Muriet lililopo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.    Katika Kilogramu 204.8165 zilizoteketezwa, mirungi ilikuwa ni Kilogramu 172.8165 na bangi kavu ilikuwa Kilogramu 32.0 yote ikihusisha jumla ya watuhumiwa 33 waliokamatwa kwa makosa ya kupatikana na dawa hizo ambapo kati yao watuhumiwa Wanaume walikuwa 25 na Wanawake walikuwa Nane ambapo wote walikamatwa katika operesheni zilizofanyika kuanzia Januari 2024 hadi Januari 27, 2025 katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.  Taratibu za uteketezaji wa vielelezo hivyo umefanyika kwa kuzingatia sheria na miongozo husika ambapo Mahakama ya Wilaya ya Arusha iliridhia vielelezo hivyo viteketezwe kwa kuwa vikikaa muda mrefu vinaweza kupoteza uhalisia na hata kupelekea kuharibika.  Aidha, Watuhumiw...

JIJI LA ARUSHA LAZINDUA MITAMBO YA BILIONI 1.7 KWA AJILI YA KUTENGENEZA BARABARA ZAKE ZOTE KOROFI ,MADIWANI WACHEKELEA HAWATABURUSHWA TENA KWENYE TOPE!

Picha
HALMASHAURI ya Jiji la Arusha imetekeleza mpango wake wa ununuzi wa Mtambo(Grader) na Magari Mawili yenye thamani ya sh, bilioni 1.7 kwa ajili ya matengenezo ya miundo mbinu ya barabara katika barabara zake zote korofi za jiji hilo. Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa malori hayo Mapya pamoja na Mtambo huo mpya mapema leo January 28,2025, iliyofanyika katika uwanja wa migambo jijini Arusha, Mkurugenzi wa jiji hilo, John Kayombo alisema, kuwa nyenzo hizo zinakwenda kuondoa Changamoto katika barabara zote katika kata 25 za jiji hilo. Aliwataka madiwani kutembea vifua mbele kwa sababu mitambo hiyo inakwenda kujibu kilio cha muda mrefu cha wananchi kwa kuondoa Changamoto ya barabara korofi. Alisema halmashauri hiyo ilitenga kiasi cha sh bilioni 2 kwa ajili ya ununuzi wa mitambo na malori ila kwa neema ya mungu tu tumeweza kununua nyenzo hizo kwa thamani ya sh, bilioni 1.7 na fedha zilizobaki zitagawanywa kwa kila kata kiasi cha sh, milioni 4 kwa ajili ya ununuzi wa vifusi. 66 "Madiwa...

KRFA YAPATA VIONGOZI WAPYA BILA KUPINGWA

Picha
Moshi.CHAMA cha Soka Mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) kimefanya uchaguzi wa viongozi wapya kwa nafasi mbalimbali, ambapo wagombea wote watakaoongoza kwa miaka minne wamepita bila kupingwa katika uchaguzi uliofanyika Jana jumapili, Januari 26, 2025, wilayani Moshi. Uchaguzi huo uliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya KRFA, Jackson Kaniki, kwa usimamizi wa wajumbe kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Khalid Mohamed, ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, na Pamela Mboya, Katibu wa Kamati hiyo. Katika mkutano huo, wajumbe 23 wamepiga kura za ndiyo kwa viongozi waliogombea nafasi tatu za Mwenyekiti, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya KRFA, huku wagombea wote wakipita bila kupingwa kwa sababu ya kukosekana wapinzani. Isaac Munis amefanikiwa kutetea nafasi yake ya Mwenyekiti wa KRFA, huku Abdalah Thabiti na Hamad Gao wakichaguliwa kuwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF. Nafasi nyingine ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya KRFA imechukuliwa n...

TANAPA YAPOKEA CHETI CHA ISO 9001:2015; YAENDELEA KUTAMBULIKA KIMATAIFA KATIKA UBORA WA HUDUMA KWA WAGENI

Picha
Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Massana J. Mwishawa, anayeshughulikia Maendeleo ya Biashara TΑΝΑΡΑ, amepokea Cheti cha ISO 9001:2015 kwa niaba ya Kamishna Mussa Nassoro Kuji, katika hafla ya iliyofanyika Januari 24, 2025 yalipo Makao Makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) jijini Arusha. Cheti hicho kilikabidhiwa kwa TANAPA na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambaye ni Dkt. Ashura Katunzi, kwa kutambua jitihada za TANAPA katika kutoa huduma kwa viwango vya kimataifa na kuimarisha huduma bora kwa wageni na wadau wanaotembelea hifadhi hizo. Hifadhi zilizopata cheti hicho ni pamoja na Ofisi ya Makao Makuu ya Shirika, Ofisi ya Kanda ya Kaskazini, Hifadhi za Taifa Kilimanjaro, Arusha, Mkomazi, Manyara na Tarangire. Utoaji wa huduma bora kwa wageni umechochea ongezeko la watalii na mapato katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Mafanikio haya pia ni matokeo ya juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mh. Rais Dkt Samia Suluhu Has...

USHIRIKI WA DCEA KATIKA UFUNGUZI WA WIKI YA SHERIA ARUSHA

Picha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini  tarehe 25.01.2025 imetoa elimu kinga dhidi ya madhara ya dawa za kulevya kwa wananchi waliohudhuria Maadhimisho ya ufunguzi wa Wiki ya Sheria mkoani Arusha yanayoendelea kuhadhimishwa katika viwanja vya TBA Kaloleni. Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria kwa Mwaka 2025 ni; *_"Tanzania ya 2050: Nafasi ya Taasisi Zinazosimamia Haki Madai Katika Kufikia Malengo Makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo"._* DCEA kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini kwa pamoja walikuwa na banda maalum la kutolea elimu ambapo Mamlaka ilichukua fursa ya maadhimisho hayo ili kuwaasa wakazi wa Mkoa wa Arusha kuachana na matumizi pamoja na biashara haramu ya dawa za kulevya lakini pia walifahamishwa kuhusu sheria kali dhidi ya wahalifu wa dawa za kulevya ambapo adhabu yake hadi kifungo cha maisha jela na mali za mtuhumiwa kutaifishwa na kuwa mali ya umma. *_Mwisho, Wananchi wali...

KAMISHNA KUJI: AHIMIZA WATUMISHI KANDA YA MAGHARIBI KUENDELEA KUWAJIBIKA KISAWASAWA KATIKA MAJUKUMU YA UHIFADHI NA USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA UTALII.

Picha
Kamishna wa Uhifadhi Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Musa Nassoro Kuji amewaasa watumishi wa TANAPA Kanda ya Magharibi kuendelea kujituma katika majukumu yao ili kuimarisha ulinzi wa Hifadhi za Taifa, ameyasema hayo leo Januari 24, 2025 katika kikao kilichofanyika ofisi za Kanda ya Magharibi, Bunda. Kamishna Kuji, aliwapongeza watumishi kwa uwajibikaji uliopelekea jana Januari 23, 2025 kupokea Tuzo ya hadhi ya juu katika kipengele cha waliosaidia kufanikisha na kurahisisha ukusanyaji wa kodi ngazi ya Taifa iliyotolewa Jijini Dar Es Salaam na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Mgeni Rasmi akiwa ni Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akizungumza katika kikao hicho Kamishna Kuji alisema "TANAPA inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa, hii inasababisha tunatambulika kitaifa na kimataifa kwa kupokea tuzo mbalimbali na Serengeti ikiwa ni kinara wa tuzo hizo, hongereni sana" Aidha, Watumishi wa kanda ya Magharibi walimshukuru Kamishna Kuji ...

𝐌𝐖𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐘𝐀𝐍𝐆’𝐀𝐑𝐀: 𝐓𝐀𝐍𝐀𝐏𝐀 𝐘𝐀𝐙𝐈𝐍𝐃𝐔𝐀 𝐊𝐀𝐌𝐏𝐄𝐍𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀 “𝐕𝐀𝐋𝐄𝐍𝐓𝐈𝐍𝐄 𝐖𝐄𝐄𝐊𝐄𝐍𝐃 𝐆𝐀𝐓𝐄𝐀𝐖𝐀𝐘 𝐍𝐀 𝐓𝐀𝐍𝐀𝐏𝐀” 𝐍𝐃𝐀𝐍𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐈𝐖𝐀 𝐂𝐇𝐀 𝐒𝐀𝐀𝐍𝐀𝐍𝐄

Picha
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa kushirikiana na Kampuni ya @busybee_cabins imezindua Kampeni yake ijulikanayo Valentine Weekend Gateway na TANAPA jana Januari 21, 2025 jijini Mwanza, lengo likiwa ni kuhamasisha Watanzania na wasio Watanzania kutembelea Hifadhi za Taifa kipindi hiki cha msimu wa Sikukuu ya Wapendanao. Akizungumzia dhima ya uzinduzi wa kampeni ya Valentine Weekend Gateaway na TANAPA, Kamishna Lyimo alisema, “Leo tunazindua kampeni hii kwa Hifadhi zote 21, tunawahamasisha Watanzania wote watembelee Hifadhi zetu maana tumeandaa vifurushi rafiki vya bei nafuu vinavyomwezesha kila Mtanzania kumudu gharama za kutalii msimu wa wapendanao.” Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Dr. Tutindaga Mwakijambile, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane, alitoa maelezo kuhusu Kisiwa cha Saanane ambapo ni mahali pa kipekee kwa wapendanao. Mandhari tulivu, fursa za kipekee za kupumzika, na shughuli mbalimbali za kuburudisha zinazotengeneza uzoefu wa kukumbukwa milele. Kamis...

_*DCEA YATOA ELIMU KATIKA ENEO LA MIGODI LA MUNDARARA ARUSHA*_

Picha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 17.01.2025 imetoa elimu kwa wananchi na wachimba madini zaidi ya 95 katika eneo la migodi ya madini aina ya rubi Mundarara wilayani Longido Arusha (M). Washiriki wa elimu hiyo walitolewa dhana potofu kuwa dawa za kulevya husababisha kupata madini mengi, bali walielimishwa kuwa dawa za kulevya zinasababisha madhara ya kiafya, kijamii na kiuchumi.  Katika mkutano huo wananchi na wachimba madini hao walihamasishwa kushirikiana na Mamlaka katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kupitia namba ya simu ya bure ya 119. *MWISHO*

DCEA KANDA YA KASKAZINI IMETEKETEZA DAWA ZA KULEVYA KILOGRAMU 185.35 ARUSHA

Picha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 15.01.2025 kwa niaba ya Kamishna Jenerali imeteketeza dawa za kulevya kilogramu 185.35 katika Dampo la Maji ya Chai liliopo wilayani Arumeru katika Mkoa wa Arusha.  Katika dawa hizo zilizoteketezwa, mirungi ilikuwa kilogramu 154.35 na bangi mbichi ilikuwa kilogramu 31 ambapo jumla  ya watuhumiwa watano walikamatwa kwa makosa ya kupatikana na dawa hizo. Uteketezaji wa dawa hizo umefanyika kwa kuzingatia taratibu zote za kisheria ambapo Mahakama ya Wilaya ya Arumeru iliridhia vielelezo hivyo viteketezwe kwani uwezekano wa kuleta madhara kwa binadamu ni mkubwa endapo  zitaendelea kuhifadhiwa. Zoezi hilo la uteketezaji umeshirikisha Maafisa kutoka Taasisi za Serikali  akiwemo  Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Afisa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkoa wa Arusha pamoja na Afisa Mazingira wa Halma...