KAMISHNA KUJI: AHIMIZA WATUMISHI KANDA YA MAGHARIBI KUENDELEA KUWAJIBIKA KISAWASAWA KATIKA MAJUKUMU YA UHIFADHI NA USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA UTALII.


Kamishna wa Uhifadhi Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Musa Nassoro Kuji amewaasa watumishi wa TANAPA Kanda ya Magharibi kuendelea kujituma katika majukumu yao ili kuimarisha ulinzi wa Hifadhi za Taifa, ameyasema hayo leo Januari 24, 2025 katika kikao kilichofanyika ofisi za Kanda ya Magharibi, Bunda.


Kamishna Kuji, aliwapongeza watumishi kwa uwajibikaji uliopelekea jana Januari 23, 2025 kupokea Tuzo ya hadhi ya juu katika kipengele cha waliosaidia kufanikisha na kurahisisha ukusanyaji wa kodi ngazi ya Taifa iliyotolewa Jijini Dar Es Salaam na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Mgeni Rasmi akiwa ni Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Akizungumza katika kikao hicho Kamishna Kuji alisema "TANAPA inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa, hii inasababisha tunatambulika kitaifa na kimataifa kwa kupokea tuzo mbalimbali na Serengeti ikiwa ni kinara wa tuzo hizo, hongereni sana"


Aidha, Watumishi wa kanda ya Magharibi walimshukuru Kamishna Kuji kwa kuendelea kutembelea na kufanya vikao na watumishi, ziara hizo zinasaidia kutatua changamoto za kiutendaji zinazowakabili watumishi pamoja na Shirika.


Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linawapongeza watumishi wa Kanda ya Magharibi kwa juhudi zao katika kuimarisha ulinzi wa hifadhi na maendeleo ya utalii. Kamishna Kuji amewaasa Maafisa na Askari Uhifadhi wa TANAPA kote nchini kuendelea kuwa waadilifu na kujituma zaidi ili kufanikisha malengo ya Shirika.

 




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE