Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2026

KRFA yachora ramani mpya ya soka Kilimanjaro, yabana mashindano holela

Picha
KRFA imepitisha maazimio ya kuimarisha maendeleo ya soka Kilimanjaro, yakiwemo kudhibiti mashindano holela (ndondo), kuzuia udanganyifu wa umri, kuibua vipaji na kuongeza waamuzi, katika mkutano mkuu wa kawaida uliofanyika Moshi. Moshi.Chama cha Soka Mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) kimekuja na ramani mpya ya maendeleo ya soka mkoani humo baada ya kupitisha maazimio kadhaa yatakayobana mashindano holela, kuibua vipaji vya vijana na kuongeza idadi ya waamuzi. Maazimio hayo yamepitishwa katika mkutano mkuu wa kawaida wa chama hicho uliofanyika Moshi, huku viongozi wakisisitiza kuwa muda wa kuendesha soka bila utaratibu umefikia mwisho. Maazimio hayo yamepitishwa katika mkutano mkuu wa kawaida wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi, huku viongozi wakisisitiza kuwa muda wa kuendesha soka bila utaratibu umefikia mwisho. Akizungumza leo Juni 1,2026 baada ya kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi,Katibu wa ...