WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI
Hai. Mchakato wa kura za maoni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Hai, Kilimanjaro, umelalamikiwa na baadhi ya wagombea na wanachama wakidai umejaa dosari ikiwemo rushwa, usafirishaji wa wajumbe na upendeleo wa wazi kutoka kwa baadhi ya viongozi. Wanachama hao wamedai kuwa licha ya chama kuwa na utaratibu wa kuhakikisha uchaguzi wa ndani unasimamiwa kwa haki, wilayani Hai kulikuwa na changamoto nyingi zenye kuondoa uhalali wa mchakato huo. Baadhi ya hoja zilizotolewa ni pamoja na majina ya wajumbe halisi kutokuwa bayana, kuruhusiwa kwa wajumbe wasio halali, huku wengine wakidaiwa kupiga kura zaidi ya mara moja. Aidha, makatibu wa kata walitajwa kushiriki kampeni za kumpigia debe aliyekuwa Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe. Katika Kata ya Machame Kaskazini, Katibu wa Kata, Silaa, alisimamishwa baada ya kudaiwa kuandika barua kwa makanisa na misikiti akihimiza wananchi kumpigia kura Mafuwe. Inadaiwa kuwa katika kata za Masama, Rundugai na Machame Mashariki, walikamatwa watu wakiw...