MEYA ATOA SAA TATU KONΤΕΝΑ LENYE UCHAFU NA HARUFU KALI YA TAKA KUONDOLEWA,ACHAFUKWA AAHIDI KUMWAJIBISHA.
MASTAHIKI Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranghe, ameweka msimamo mkali dhidi ya uzembe katika usimamizi wa usafi wa mazingira jijini humo, akiahidi kumwajibisha Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, James Lebikoki, kwa kushindwa kusimamia ipasavyo watendaji wake hali iliyosababisha kuendelea kwa kero ya uchafu, hususan katika masoko ya jiji. Akizungumza leo Januari 4, 2026 wakati wa ziara ya kampeni ya "Ng'arisha Jiji" katika Soko la Mitumba Mbauda, kata ya Sombetini, Meya Iranghe alisema suala la usafi si mjadala wa kisiasa bali ni wajibu wa kiutendaji, akionya kuwa hatasita kuchukua hatua kali dhidi ya viongozi na watendaji wanaoshindwa kutimiza majukumu yao. Iranghe alionekana kukerwa na harufu kali na mrundikano wa taka ngumu zilizokuwa zimejaa kwenye kontena la soko hilo, hali ambayo wafanyabiashara walieleza kuwa taka hizo hukaa kwa zaidi ya wiki mbili, kunyeshewa na mvua na kuhatarisha afya zao kutokana na uwezekano wa magonjwa ya mlipuko. Katika hotuba yake, Me...