MEYA ATOA SAA TATU KONΤΕΝΑ LENYE UCHAFU NA HARUFU KALI YA TAKA KUONDOLEWA,ACHAFUKWA AAHIDI KUMWAJIBISHA.


MASTAHIKI Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranghe, ameweka msimamo mkali dhidi ya uzembe katika usimamizi wa usafi wa mazingira jijini humo, akiahidi kumwajibisha Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, James Lebikoki, kwa kushindwa kusimamia ipasavyo watendaji wake hali iliyosababisha kuendelea kwa kero ya uchafu, hususan katika masoko ya jiji.


Akizungumza leo Januari 4, 2026 wakati wa ziara ya kampeni ya "Ng'arisha Jiji" katika Soko la Mitumba Mbauda, kata ya Sombetini, Meya Iranghe alisema suala la usafi si mjadala wa kisiasa bali ni wajibu wa kiutendaji, akionya kuwa hatasita kuchukua hatua kali dhidi ya viongozi na watendaji wanaoshindwa kutimiza majukumu yao.

Iranghe alionekana kukerwa na harufu kali na mrundikano wa taka ngumu zilizokuwa zimejaa kwenye kontena la soko hilo, hali ambayo wafanyabiashara walieleza kuwa taka hizo hukaa kwa zaidi ya wiki mbili, kunyeshewa na mvua na kuhatarisha afya zao kutokana na uwezekano wa magonjwa ya mlipuko.

Katika hotuba yake, Meya alisema haiwezekani mapambano ya usafi wa mazingira yakabaki kuwa jukumu lake pekee, huku baadhi ya watendaji waliokabidhiwa dhamana hiyo wakishindwa kumuunga mkono kwa vitendo.


Alieleza kuwa alipokabidhiwa uongozi, Jiji la Arusha lilikuwa likishika nafasi ya mwisho kwa uchafu, lakini kupitia juhudi na msimamo wake, kwa sasa limepiga hatua na kufikia nafasi ya pili kwa usafi, hatua ambayo alisema haipaswi kurudishwa nyuma kwa uzembe wa baadhi ya wahusika.

"Siwezi kupambana peke yangu. Nimekuta Jiji la Arusha likiwa la mwisho kwa uchafu, sasa hivi tumepanda hadi nafasi ya pili kwa usafi. Haiwezekani katika mapambano haya nibaki mwenyewe huku wengine wakidai nㅈta umaarufu. Hapa hakuna siasa, hii ni kazi," alisema Iranghe


Alisisitiza kuwa dhamana aliyopewa ni ya kuwatumikia wananchi, si kujijenga kisiasa, akionya kuwa atawawajibisha wote watakaokwaza juhudi za kufanya Arusha kuwa jiji safi na salama kiafya.

"Hii ni kazi mmenipa, lazima niwatumikie wananchi. Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, usipowajibika awamu hii, nitakuwajibisha," alionya kwa msisitizo.

Akiendelea kutoa maelekezo, Meya aliagiza kuitishwa kwa kikao cha maafisa tarafa na mawakala wa ukusanyaji taka, ili kubaini sababu za uzembe katika usimamizi wa usafi wa mazingira jijini.

Pia alimuelekeza Katibu wa Soko kusimamia kikamilifu kanuni za usafi, akitangaza kuwa ni marufuku kufanya biashara bila kufanya usafi, na kwamba baada ya shughuli za biashara, usafi ufanyike mara moja.

Aidha, Iranghe alielekeza utozwaji wa faini kwa wote wanaokiuka sheria za usafi uendelee bila kusita, na kwa waendelezao ukaidi wachukuliwe hatua kali ikiwemo kuondolewa sokoni, ili kupisha wafanyabiashara wanaoheshimu sheria na kanur "izopo.






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE