DCEA YAFANYA MAFUNZO MAALUM YA KUWAJENGEA UWEZO WADAU WA ASASI ZA KIRAIA MKOANI ARUSHA*_
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 24.09.2025 ilifanya mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa Asasi 5 za kiraia ambazo ni Bluecross Society of Tanzania, Care for All, Vision of Hope, Siha Angavu na YEPAO juu ya utambuzi wa awali, ushauri nasihi na uunganishaji wa mraibu katika huduma za matibabu (Screening, Brief Intervention, and Referral to Treatment-SBIRT) katika Ukumbi wa Asasi ya Bluecross iliyopo Sakina jijini Arusha. Aidha, wawakilishi hao waliekezwa mbinu zilizothibitishwa kisayansi za utambuzi wa vijana ambao tayari wameshaanza kutumia dawa za kulevya, jinsi ya kuwashauri wasitishe matumizi hayo pamoja na jinsi ya kuwaunganisha katika huduma sahihi za matibabu yanayopatikana maeneo ya karibu wanapoishi. Pia, walihamasishwa kuendelea kushirikiana na Mamlaka kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kupitia namba ya simu ya bure ya 119. *MWISHO*