Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2025

MATI SUPER BRANDS YADHAMINI MASHINDANO YA WEST KILI TOUR CHALLENGE 2025

Picha
 Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited imedhamini mashindano ya West Kili Tour Challenge 2025 msimu wa 5 yanayojumuisha mbio za riadha,baiskeli na piki piki yaliyofanyika katikati ya Hifadhi ya shamba la Miti la West Kilimanjaro kwa lengo la kukuza utalii wa michezo na kuunga mkono juhudi za Rais Dr.Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii kupitia filamu ya Royal Tour. Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Kampuni hiyo Brayson Mnene amesema wamekua wakidhamini mashindano hayo kwa miaka miwili mfululizo kwa lengo la kuunga mkono utalii wa michezo na shughuli za uhifadhi zinazofanywa kwa lengo la kutunza ekolojia ya Mlima Kilimanjaro. Mkuu wa Wilaya ya Siha Dr.Christopher Timbuka amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kufanya utalii katika hifadhi ya shamba la miti la West Kilimanjaro lenye vivutio mbali mbali vya utalii ikiwemo wanyamapori,ndege na miti ya asili.   Mkuu wa Hifadhi ya West Kilimanjaro Robert Faida ameyataka makampuni mbali mba...

MBUNGE WA JIMBO LA MONDULI FRED LOWASA AMPONGEZA BILIONEA MULOKOZI KWA KUTOA MSAADA WA VITI MWENDO KWA WATU WENYE ULEMAVU

Picha
Mbunge wa Jimbo la Monduli Fred Lowasa amempongeza Mfanyabiashara maarufu Bilionea David Mulokozi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mati Super Brands kwa kutoa misaada mbali mbali kwa watu wenye ulemavu ikiwemo viti mwendo kupitia Taasisi yake ya Mati Foundation. Akizungumza katika kata ya Makuyuni Wilayani Monduli mkoani Arusha kwenye Halfa ya kukabidhi misaada kwa watu wenye ulemavu ikiwemo viti mwendo ,vifaa vya shule pamoja na gesi zilizotolewa na shirika lisilokua la kiserikali la SYWSO kwa ufadhili wa taasisi ya MATI FOUNDATION iliyoanzishwa na Bilionea Mulokozi kwa lengo la kusaidia jamii . Lowasa amempongeza David Mulukozi kwa kuwa mfano bora wa kuigwa kwa kutumia sehemu ya faida anayoipata kwenye biashara zake kusaidia jamii ya Watanzania. Aidha Mbunge huyo amewataka Watanzania kumuenzi kwa vitendo Dr.Reginald Mengi kwa kuwawezesha watu wenye Ulemavu kijamii na kiuchumi huku akimtaka Mfanyabiashara Bilionea David Mulokozi kuendeleza kazi nzuri alizozifanya Mengi kwa ...

HALMASHAURI WASICHUKUE VISHIKWAMBI WALIVYOKUWA WANATUMIA MADIWANI WANAOMALIZA MUDA - MCHENGERWA

Picha
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa, amemwangiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo Adolf Ndunguru kuwaandikia wakurugenzi wa Halmashauri kutokuchukua vishikwambi walivyokuwa wanatumia madiwani waliomaliza muda wao pamoja na stahiki zao. Akizungumza kwa njia ya simu  leo 20 Juni, 2025, baada ya kupigiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, Waziri Mchengerwa amesema kuwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia yametekelezwa vyema kupitia usimamizi madhubuti wa Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. "Ni kazi ya nguvu, jasho, ubunifu na stadi za madiwani kote nchini. Nawapongeza Mameya wote kwa kazi yao kubwa, hususan Meya wa Jiji la Arusha. Kazi yao imeandikwa katika kitabu cha dhahabu kwa kuwa wamewahudumia wananchi wanyonge kwa moyo wa uzalendo," amesema Mhe. Mchengerwa. Katika hatua nyingine, Waziri Mchengerwa ametumia nafasi hiyo kumpongeza Mkuu wa Mko...

WANAKIJIJI HEIKONTI SAME KWA HIARI WAAMUA KUNG’OA VISIKI VYA MIRUNGI; DCEA YASHIRIKI ZOEZI HILO

Picha
Wananchi wa Kata ya Tae, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) pamoja na Serikali ya Wilaya ya Same tarehe 30.05.2025 wameshiriki zoezi la kung’oa visiki vya mimea ya dawa za kulevya aina ya mirungi iliyopandwa katika Kijiji cha Heikonti kilichopo ndani ya Kata ya Tae wilayani Same. Hamasa ya wananchi wa kijiji hicho kwa hiari wameamua kung’oa visiki vya mirungi kufuatia elimu waliyoipata kutoka katika mamlaka za Serikali ikiwemo DCEA katika kutafuta suluhu ya kukabiliana na kilimo cha dawa za kulevya aina ya mirungi ambapo tayari Serikali imeshapata mazao mbadala zaidi ya nane kwa Wanakijiji wa Kata za Tae, Vudee na maeneo mengine ambayo hapo awali yalishamiri kwa kilimo cha mirungi. Sehemu ya visiki vya mirungi vilivyong’olewa kwa hiari na wananchi katika Kijiji hicho inatokana na operesheni kubwa ya uteketezaji wa mashamba ya mirungi iliyofanyika Mwezi Machi 2025 chini ya usimamizi wa Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas Lyimo katika Vijiji na Vitongoji vilivyopo...