Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2024

KIVUTIO CHA UTALII UHAMAJI WA NYUMBU NI ZAO LA UTAFITI

Picha
Ikiwa tarehe 27 Septemba kila mwaka Mataifa mbalimbali huadhimisha Siku ya Utalii Duniani, Tafiti za Wanyamapori zimeendelea kuchangia kukua kwa Utalii ambapo ugunduzi wa Kivutio kikubwa cha Utalii cha tukio la kiasili la Uhamaji wa Nyumbu (The Great Migration) ni zao la Utafiti.  Mtafiti wa Nyumbu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Dkt. Emmanuel Masenga amesema tafiti za wanyamapori zimechochea kuimarika kwa uhifadhi na kukuza utalii ambapo kivutio cha kuhama kwa nyumbu ndani ya hifadhi ya Taifa Serengeti ni zao la tafiti za miaka ya 1950 "Mtafiti Prf. Bernard Grzimek ndie mgunduzi wa kivutio hiki" amebainisha Dkt. Masenga. Aidha, Dkt. Masenga amesema mbali na ugunduzi wa kivutio cha kuhama kwa Nyumbu, TAWIRI imeendelea kufanya tafiti mbalimbali zinazolenga kuimarisha uhifadhi wa nyumbu ambapo zimesaidia kubaini na kuhifadhi maeneo wanayozaliana kwenye mbuga za nyasi fupi kusini mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Pori la Akiba M...

RAIS SAMIA AZINDUA SOKO LA MADINI YA VITO NA DHAHABU TUNDURU

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan* amezindua Soko la Madini ya Vito na Dhahabu Wilayani Tunduru ikiwa ni moja ya shughuli alizofanya akiwa katika ziara ya kikazi ya siku 6 Mkoani Ruvuma.  "Kwa dhati kabisa, napenda kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa utekelezaji wa Sera ya kushirikiana na sekta binafsi yaani Public Private Partnership kwa vitendo ambapo Serikali imeweka fedha kiasi na kiasi kingine kimechangiwa na wafanyabiashara wa madini waliopo hapa Wilayani Tunduru" "Ni dhahiri kwamba ujenzi wa soko hili kubwa na la kisasa utarahisisha biashara ya madini Wilayani hapa na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji maduhuli ya Serikali sambamba na kudhibiti udanganyifu na utoroshaji wa madini", alibainisha Mhe. Rais. Aidha, Rais Samia ameonesha wazi kufurahishwa na ushirikiano huo wa Halmashauri na Sekta binafsi na kusisitiza kwamba Sera ya PPP ikitelezwa kwa vitendo ni chachu ya maendeleo ya wananchi katika Wilaya zote n...

WANANCHI 119 KUTOKA ENEO LA HIFADHI YA NGORONGORO WAPOKELEWA NA KUKABIDHIWA MAKAZI YAO MSOMERA

Picha
Jumla ya kaya 26 zenye watu 119 na mifugo 300 zilizokubali kuhama kwa hiari kutoka ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro zimepokelewa rasmi katika Kijiji Msomera, Wilayani Handeni Tanga tarehe 28 Septemba, 2024.  Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Katibu tarafa wa tarafa ya Sindeni Bw. Baraka Nkatura alisema kwamba Serikali imejipanga vizuri kuhakikisha kuwa wananchi hao waliokubali kuhama kwa hiari wanapatiwa huduma bora kama walivyoahidiwa.  “Leo tumewapokea rasmi, mtakabidhiwa makazi yenu mapya yaliyoandaliwa na Serikali ambako mtapewa nyumba yenye vyumba vitatu iliyojengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa hekari 2.5, kuna maeneo yaliyotengwa mahususi kwa ajili ya shughuli za malisho na kilimo ambayo mtaonyeshwa na wataalamu wetu ndani ya siku chache zijazo” alisema Baraka Akiongoza zoei la kugawa nyumba Msimamizi msaidizi wa ujenzi wa nyumba Msomera kwa upande wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bw. Faudhi Bossa alieleza kuwa ujenzi wa nyumba 2,500 kwa Kiji...

DCEA YATOA ELIMU KINGA JUU YA MADHARA YA TATIZO LA DAWA ZA KULEVYA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA TURKISH MAARIF JIJINI ARUSHA

Picha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Asasi ya Youth and Community Rehabilitation (YCR) na Drug Abuse and Recovery Organization (DARO) tarehe 25.09.2024 imetoa elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya katika shule ya sekondari Turkish Maarif iliyopo Ngaramtoni Arumeru (W) Arusha (M). Aidha, elimu hiyo ilitolewa kwa wanafunzi zaidi ya 230 ikiwa na lengo la kuwapa elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya pamoja na kuwapa mbinu wanazopaswa kuzitumia ili waweze kujikinga na matumizi ya dawa za kulevya. Ofisi ya Mamlaka Kanda ya Kaskazini itaendelea kushirikiana na Asasi za Kiraia katika utekelezaji wa majukumu yake kwa lengo la kuwawezesha na kuimarisha mashirikiano ambayo tunaamini yatasaidia kueneza elimu zaidi kwa jamii ili tuweze kupata matokeo yenye tija zaidi.

DCEA YAPIGA HODI WILAYANI MWANGA; YATOA ELIMU KINGA KWA WANAFUNZI NA JAMII SOKONI MWANGA

Picha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya Wilaya ya Mwanga tarehe 19.09.2024 imetoa elimu kinga kwa makundi mbalimbali  juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.  Jumla ya watu 2,500 walipatiwa elimu kinga ikihusisha wanafunzi wa Shule za Sekondari za Mwanga, Vudoi na Mandaka pamoja na wafanyabiashara/wachuuzi wa  Soko la Mwanga. DCEA Kanda ya Kaskazini iliwahamasisha wananchi  wa Wilaya ya Mwanga washirikiane na Mamlaka katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya waliopo katika maeneo yao wanayoishi kwa kupiga bure namba ya simu 119.

TUME YA MADINI YAPATA MKURUGENZI MPYA WA HUDUMA ZA TUME

Picha
Leo Septemba 19, 2024 aliyekuwa Mkurugenzi wa Huduma za Tume, CPA. William Mtinya amekabidhi Ofisi kwa Nsajigwa Kabigi aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Afya. Akizungumza kwenye ofisi za makao makuu ya Tume ya Madini jijini Dodoma mbele ya Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, aliyekuwa Mkurugenzi wa Huduma za Tume, CPA William Mtinya ameshukuru watendaji wa Tume ya Madini kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha tangu aliposhika nafasi hiyo na kuwataka kuendelea kumpa ushirikiano Kaimu Mkurugenzi mpya wa Huduma za Tume. Naye Kaimu Mkurugenzi Mpya wa Huduma za Tume, Nsajigwa Kabigi ameomba watumishi wote wa Tume ya Madini kuendeleza ushirikiano ili kuhakikisha Sekta ya Madini inaendelea kuwa na mchango mkubwa kwenye Pato la Taifa. Amesisitiza kuwa Ofisi yake itaendelea kutatua changamoto mbalimbali sambamba na kuboresha mazingira ya ofisi zote za madini nchini kwa kuhakikisha zinapata vitendea kazi ili kutoa huduma za ...

UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA DCEA WILAYANI SIHA KILIMANJARO

Picha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) tarehe 18.09.2024 imetoa elimu kinga kwa jamii juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya wilayani Siha Mkoa wa Kilimanjaro.  Jumla ya watu takribani 1,400 walipatiwa elimu hiyo ikihusisha madereva wa magari madogo, wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Namwai,Matadi na Askari wa Jeshi la Akiba la Mgambo pamoja na wananchi na wafanyabiashara wa Soko la Sanya Juu.  DCEA Kanda ya Kaskazini iliwahamasisha wananchi wa wilaya ya Siha washirikiane na Mamlaka katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa hizo wanaopatikana katika maeneo yao wanayoishi kwa kupiga namba ya simu ya bure ya 119.

UJENZI WA KIWANDA CHA CHUMVI WA AANZA LINDI

Picha
Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa Ujenzi wa Kiwanda cha kusafisha madini ya chumvi kinachojengwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) katika eneo la Lingaula Wilayani Kilwa ni utekelezaji wa ahadi ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa kwa wakulima wa chumvi alipofanya ziara yake Mkoani Lindi. Amebainisha hayo leo Septemba 18, 2024 alipotembelea eneo patakapojengwa kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na kupokea rasmi Hati ya umiliki wa ardhi wa eneo hilo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi. Mhe. Mavunde amesema kuwa anamshukuru *Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* kwa kusikia kilio cha wakulima wa chumvi juu ya ukosefu wa masoko ya uhakika, hatua iliyopelekea kutupa maelekezo ya kuhakikisha tunasimamia ujenzi wa kiwanda hiki haraka ili kutatua kero hiyo ya muda mrefu kwa wakulima wa chumvi  wa maeneo mengi nchini ikiwemo wa Mkoa wa Lindi. “Mhe. Rais alipokuja kwenye ziara yake katika Mkoa huu, moja kati ya mambo aliyoyasikia na kupokea ni kilio cha Wazalishaji w...

SERIKALI YAENDELEA KUTIMIZA AHADI YA KUGAWA MAHINDI KWA WANANCHI WA NGORONGORO WALIOHAMIA MSOMERA.

Picha
Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeendelea kutimiza ahadi ya kugawa chakula kwa wananchi waliotoka eneo la hifadhi ya Ngorongoro na kuhamia kijiji cha msomera kwa kuwapa gunia 2 za mahindi kila kaya ambapo mpango huo hufanyika kila baada ya miezi mitatu kwa kipindi cha miezi 18 wakiwa wanaendelea kuzoea mazingira. Akiongoza zoezi la ugawaji wa mahindi tarehe 18/09/2024, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa uhifadhi anayesimamia idara ya Maendeleo ya Jamii Gloria Bideberi, alisema kuwa zoezi la ugawaji wa mahindi kwa wananchi hao ni endelevu na linafanyika kila baada ya miezi mitatu kwa kadri wananchi wanavyoendelea kuhamia katika Kijiji cha Msomera.  “Sisi kama Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro tunaendelea na utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhakikisha kuwa kila mwananchi wa Ngorongoro aliyehamia Msomera pamoja na nyumba na huduma nyingine ambazo anapewa na Serikali, tunahakikisha pia anapatiwa Mahindi jumla ya magunia 12 kwa muda wa Miezi 18 ya mwanzo akiwa...

WAZIRI MCHENGERWA AAGIZA SHULE ZA WASICHANA ZA SAMIA KUKAMILIKA KWA WAKATI.

Picha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa ameziagiza mamlaka zote za Mikoa na wilaya nchini kuhakikisha kuwa shule zote 26 zinazojengwa maalum kwaajili ya masomo ya Sayansi kwa wasichana zinakamilika kwa wakati na kwa ubora kulingana na thamani ya fedha itakayotumika. Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Septemba 18, 2024 alipoambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule ya Sekondari Longido Samia na kuagiza shule hiyo kukamilika ifikapo Novemba Mosi mwaka huu. Mhe. Mchengerwa amefikia hatua hiyo mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Makonda kueleza kuwa ripoti ya awali ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa Mkoa wa Arusha kubainisha kuwa zaidi ya Shilingi Bilioni 1. 3 utekelezaji wa mradi huo zimetumika nje ya mfumo halali wa matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo. Rc Makonda amesema Shilingi bilioni 1 zilitumika pasipo kupitia mfumo wa kieletroniki wa EFDs laki...

WAZIRI MCHENGERWA ATAKA UDHIBITI WA HOMA YA NYANI MIKOA YA MIPAKANI.

Picha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaagiza wakuu wote wa mikoa ya pembezoni mwa nchi kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa mipakani kujilinda na Homa ya nyani kuweza kuingia nchini. Mhe. Mchengerwa ametoa maagizo hayo leo Jumatano Septemba 18, 2024 mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Longido Mkoani Arusha akitahadharisha kuchukua hatua kwa Mamlaka za Wilaya na Mikoa itakayozembea na kusababisha ugonjwa huo kuingia nchini Tanzania. "Ugonjwa huu hauko mbali,upo jirani tu kwahiyo msingi huu wa kuimarisha ulinzi katika mipaka yetu itatusaidia kutambua yule anayeingia lazima afanyiwe uchunguzi wa kiafya kwa mujibu wa namna taratibu za wenzetu wizara ya afya walivyotupatia." Amesema Mhe. Mchengerwa. Mhe. Mchengerwa kadhalika ameahidi kuzungumza na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba katika kuhakikisha kuwa kunafungwa mashine za ukaguzi kwenye kituo cha Naman...

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA GREEN HIPPO TRAVELS AZURU MAKUYUNI WILDLIFE PARK

Picha
Mkurugenzi wa Kampuni mashuhuri ya utalii inayofahamika kama Green Hippo Travels, Astrid Kleinveld akiwa ameambatana na rafiki yake Naomi Rugenbrink ambao wote ni raia wa Uholanzi, tarehe 15 septemba 2024, walitembelea eneo la Makuyuni Wildlife Park liliopo wilayani Monduli mkoani Arusha kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo na kupata fursa ya kufahamu namna wanavyoweza kufanya biashara ya utalii katika eneo hili hasa utalii wa Kupanda Mlima na Kutembea kwa miguu. Bi Astrid na mwenzake wakiongozwa na Afisa Utalii wa eneo hilo Chacha Masase walipata fursa ya kupanda Mlima Kipara ambao unapatikana ndani ya eneo hilo wenye urefu wa mita 1900 kutoka usawa wa bahari pamoja na kufanya utalii wa Kutembea kwa miguu hivyo kufanikiwa kuona wanyamapori kwa ukaribu zaidi na kufurahia mandhari iliyopo. "Uzuri wa eneo hili ni wa kustaajabisha mnoo, tumepata uzoefu wa kipekee ambao nina imani sio sisi tu bali mtalii yeyote atakae kuja ataifurahia Makuyuni Wildlife Park kuanzia mapokezi ya w...