KIVUTIO CHA UTALII UHAMAJI WA NYUMBU NI ZAO LA UTAFITI


Ikiwa tarehe 27 Septemba kila mwaka Mataifa mbalimbali huadhimisha Siku ya Utalii Duniani, Tafiti za Wanyamapori zimeendelea kuchangia kukua kwa Utalii ambapo ugunduzi wa Kivutio kikubwa cha Utalii cha tukio la kiasili la Uhamaji wa Nyumbu (The Great Migration) ni zao la Utafiti. 

Mtafiti wa Nyumbu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Dkt. Emmanuel Masenga amesema tafiti za wanyamapori zimechochea kuimarika kwa uhifadhi na kukuza utalii ambapo kivutio cha kuhama kwa nyumbu ndani ya hifadhi ya Taifa Serengeti ni zao la tafiti za miaka ya 1950 "Mtafiti Prf. Bernard Grzimek ndie mgunduzi wa kivutio hiki" amebainisha Dkt. Masenga.

Aidha, Dkt. Masenga amesema mbali na ugunduzi wa kivutio cha kuhama kwa Nyumbu, TAWIRI imeendelea kufanya tafiti mbalimbali zinazolenga kuimarisha uhifadhi wa nyumbu ambapo zimesaidia kubaini na kuhifadhi maeneo wanayozaliana kwenye mbuga za nyasi fupi kusini mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Pori la Akiba Maswa, na Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro. Pia tafiti zimesaidia kuhifadhi maeneo ya mapito/Shoroba hivyo uhamaji huo kuwa endelevu.

Vilevile, kwa upande wa utalii uhamaji wa nyumbu ni kivutio cha kipekee cha Utalii na tafiti zimesaidia kushauri namna bora ya kufanya utalii Kaskazini mwa Hifadhi yaTaifa Serengeti maeneo ya Mto Mara sambamba na kutoa takwimu zinazotumika kunadi Utalii "takwimu za sensa hutumika kutangaza utalii ambapo kwa mujibu wa ripoti ya sensa ya 2023, Mfumo Ikolojia wa Serengeti una jumla ya Nyumbu 1,579,850" ameeleza Dkt.Masenga





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE