Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2024

WAZIRI MKUU MAJALIWA APONGEZA MCHANGO WA SEKTA YA MADINI NCHINI

Picha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameipongeza Wizara ya Madini kwa juhudi mbalimbali inazofanya za kuiendeleza Sekta ya Madini kufikia asilimia 9.0 katika kuchangia kwenye Pato la Taifa huku sekta ikikua kwa asilimia 11.3. Ameyasema hayo, leo Novemba 19, 2023 wakati wakufungua Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini 2024 unaendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa uwepo wa Sera nzuri zenye ushawishi mazingira  salama yenye utulivu na amani uwepo wa masoko ya uhakika yaliyounganishwa na jiografia nzuri vyote hivyo kwa pamoja vimekuwa vichocheo vikubwa katika ukuaji wa Sekta ya Madini nchini. Waziri Mkuu Majaliwa amefafanua kuwa  Serikali itaendelea kuboresha miundombinu yote inayohusiana na mnyororo mzima wa thamani madini ikiwa barabara nishati ya umeme pamoja na kuongeza idadi ya  vituo vya mauzo na masoko ili kuiweka sekta katika hali ya  ...

*Misaada kwa ajili ya waathirika wa kuporomoka kwa jengo Kariakoo itolewe kwenye akaunti moja- Dkt. Yonazi*

Picha
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema msaada wa kifedha kwa ajili ya kusaidia walioathirika na kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo Jijini Dar es Salaam unatolewa kwa akaunti maalum ya maafa ya 9921159801 ambayo ipo Benki Kuu ya Tanzania na kushughulikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu. Dkt. Yonazi ameyasema hayo leo Novemba 18, 2024 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hali inayoendelea katika zoezi la uokoaji. Amesema akaunti hiyo ni pekee nchini ambayo inakusanya misaada ya kifedha kwa ajili ya maafa. "Kuna watu wana nia njema kabisa ya kuwasaidia Watanzania, lakini naomba tujizuie kabisa kukusanya michango ya kifedha kutoka kwa mtu yeyote bila kupitia akaunti hii". Amesema Dkt. Yonazi. Aidha amesema akaunti hiyo ni maalumu imethibitishwa na serikali ili kuweza kuhakikisha misaada inawafikia walengwa na inatimiza malengo ya kutoa misaada hiyo. Amesema kwa sasa operesheni inaendelea mpaka pale wa...

MKUTANO WA KIMATAIFA SEKTA YA MADINI KUONGEZA FURSA ZA UWEKEZAJI TANZANIA*

Picha
Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini unatarajiwa kuongeza fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini hapa nchini sambamba na kuweka msingi thabiti wa ushirikiano baina ya wadau, kuimarisha uzalishaji wa madini, na kuhakikisha kuwa rasilimali za madini zinawanufaisha watanzania kiuchumi na kijamii. Amesema hayo leo Novemba 14, 2024 wakati akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya Mkutano wa 6 wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini Tanzania, unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 19 hadi 21 Novemba 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.  Amesema kuwa, Mkutano huo unaoongozwa na Kaulimbiu ya “Uongezaji Thamani Madini kwa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii” unatarajiwa kuvutia zaidi ya washiriki muhimu Zaidi ya 1,500 kutoka Tanzania na nchi mbalimbali duniani na kwamba ni jukwaa muhimu kwa wadau wa madini k...

NMB foundation wampatia ufadhili mwanafunzi IAA.

Picha
Arusha. Mwanafunzi Selesi John Njacha anaesoma chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) amefanikiwa kupata ufadhili wa masomo pamoja na msaada wa vifaa kupitia mpango wa ‘NMB nuru yangu Scholarship and Mentorship’ inayotolewa na Asasi ya Kiraia ya NMB Foundation. Selesi anaesoma Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Usalama wa Mtandao (Cybersecurity) mwaka wa pili amepata ufadhili huo utakaojumuisha malipo yote ya ada, nauli, posho, vifaa vya kusomea na kuandikia(stationary), mafunzo ya vitendo ‘field’ na laptop. Akibidhi vifaa hivyo vya kujifunzia leo Novemba 13,2024 jijini Arusha, Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini, Baraka Ladislaus amesema kuwa Mwanafunzi huyo atalipiwa malipo yote yatakayolewa na shule kwa miaka yote ya shahada ya kwanza pamoja na vifaa vya kujifunzia. “Ufadhili huu unaotolewa na Asasi ya Kiraia ya ‘NMB Foundation’ iliyo chini ya Benki ya yetu, unatolewa kwa wanafunzi wanaojiunga chuo katika fani za Hesabu na Takwimu, Biashara, Uchumi, Teknolojia, Habari na Mawasiliano, Uhasibu,...

ALIYOSEMA WAZIRI WA MADINI MHE. ANTHONY MAVUNDE KATIKA MAHOJIANO MAALUM NA CROWN MEDIA KUPITIA KIPINDI CHA KASRI LA KIKEKE NOVEMBA 12, 2024

Picha
Ukiuza Madini Nje ya Soko wewe ni mtoroshaji* Tulikuwa na changamoto ya biashara ya Madini kabla ya mwaka 2017 ambapo ilifanyika kiholela kutokana na kukosekana kwa masoko ya madini. Hivi sasa biashara yote inafanyika sokoni, ukiuzia nje ya Soko wewe ni mtoroshaji unakiuka Sheria za nchi na kupoteza mapato ya Serikali.   *Tozo kwenye uchimbaji mdogo* Nimefanya vikao na wadau mbalimbali kusikiliza hoja zao lengo ni kuangalia namna ya kutatua changamoto kwenye shughuli za uchimbaji mdogo wa madini na biashara ya madini. Hivi sasa kodi zote zinazolipwa Serikalini zimebaki asilimia 9.3 kutoka 38. Mrabaha ni asilimia 6, ada ya ukaguzi asilimia1, TRA asilimia 2 (withholding tax) na Service levy asilimia 0.3. Serikali imechukua hatua kubwa kusikiliza changamoto za wachimbaji wadogo, kodi inayokusanywa inasaidia kujenga nchi yetu. *Mkakati wa Kuongeza Thamani Madini Nchini* Kwenye hotuba yangu ya Bajeti nilieleza kuhusu mpango wa Serikali kutoendelea kutoa Leseni za uchimbaji mkubwa wa mad...

AU YAIPATIA TANZANIA DOLA ZA KIMAREKANI 200,000 MCHANGO MAAFA HANANG

Picha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, na Uratibu) Mhe. William Lukuvi ameishukuru Umoja wa Afrika kwa kutoa kibali cha kuichangia nchi ya Tanzania Dola za Kimarekani 200,000 kama ishara ya mshikamano kutokana na maafa makubwa yaliyotokea Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara.   Waziri Lukuvi ametoa shukrani hizo leo tarehe 12 Novemba, 2024 katika Ofisi za Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu zilizopo Jijini Dodoma na kubainisha kuwa mchango huo ni muhimu kwa kuwa utasaidia juhudi zinazofanywa na Serikali za kurejesha hali ikiwemo ujenzi wa shule, kituo cha afya na soko katika eneo lililoathirika.   Akipokea mchango wa fedha hizo kutoka kwa Mheshimiwa Balozi Tabelelo Alfred Boang, Balozi wa Jamhuri wa Muungano wa Botswana nchini Ethiopia na Mwakilishi wa kamati ya Mabalozi (Permanent Representative Sub Committee on refugees, Returnees and IDPs), Mhe. Lukuvi amemweleza kuwa, mwaka 2023/2024 Tanzania ilikumbwa na El-Niño ambayo ilisababisha kuwepo kwa mvua kubwa zilizofululi...

📍ASANTENI ARUSHA(WALIMU, WAFANYAKAZI NA SHULE ZOTE ZISIZO ZA SERIKALI MKOA WA ARUSHA

Picha
Tunawashukuru walimu na wafanyakazi wa shule za notre dame na canossa kwa kukipokea chama chenu cha TPTU na kujiunga nacho. Tunalishukuru jimbo kuu katoliki la Arusha, kwa ushirikiano wenu wa dhati kwa chama cha TPTU, kwa kushirikiana nasi na kutuunganisha na shule zenu zote za jimbo kuu la Arusha, ili tuweze kutekeleza takwa la kisheria la kukutana na kuzungumza na kuwasajili uanachama walimu na wafanyakazi wa shule zenu. Tunawashukuru shule zote zisizo za serikali kwa ujumla wake mkoa wa Arusha, kwa ushirikiano wenu kwa kadri tunavyowafikia mmoja mmoja, shabaha yetu kuu ni kujenga ustawi bora kwa shule zote zisizo za serikali nchini, walimu na wafanyakazi wake wote kwa ujumla wao. Aidha tunapenda kuwafahamisha kuwa , kwa mkoa wa Arusha, ofisi zetu za chama cha TPTU zinapatikana jengo la NSSF(uzunguni) orofa ya kwanza, chini ya katibu wetu wa chama cha TPTU mkoa wa Arusha, taaluma mwanasheria, Bi Aika kweka, simu 0763143442 na 0784719109, tunawakaribisha sana ofisini kwetu kwa ufafanu...

TZLPGA YAENDELEA KUTOA ELIMU MATUMIZI YA NISHATI SAFI

Picha
Chama cha waagizaji na wasambazaji wa gesi ya mitungi chini(TZLPGA) kinaendelea na utoaji wa Elimu kwa wananchi ili watumie Nishati safi ya kupikia ili kufikia lengo la Serikali ifikapo Mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania wanatumia Nishati safi. Taarifa hiyo imetolewa Novemba 8,2024 na Mkurugenzi Mkuu wa Chama hicho Amos Jackson Mwansumbule wakati, akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake  Jijini Dar es salaam. Amesema kuwa Elimu kuhusu matumizi ya nishati safi itokanayo na gesi asilia imekua changamoto kubwa kutokana na wananchi wengi bado wanatumia Nishati chafu(mkaa na kuni) ambayo inaathiri afya zao pamoja na kusababisha uharibifu wa Mazingira. Aidha amesema kuwa changamoto nyingine ni gharama ya mitungi ya gesi,ambapo watu wengi wamekua wakitumia sababu hiyo kama sababu ya kutotumia nishati safi itokanayo na gesi asilia kwa madai kuwa hawana uwezo wa kutumia gesi. " Hii gesi tunaitoa nje ya nchi,tunainunua kwa gharama ya bei ya soko la Dunia,kwa maana hiyo kuna ghara...

WAFUGAJI ARUSHA WAPEWA ELIMU YA UFUGAJI NYUKI

Picha
Zaidi ya wafugaji 100 wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha wamenufaika na mafunzo ya ufugaji bora wanyuki, uongezaji thamani mazao ya nyuki, uchakataji wa sumu ya nyuki na uandaaji wa maziwa ya nyuki (Royal Jelly) . Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya Mafunzo hayo yaliyotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) wafugaji hao wameshukuru kujengewa uwezo wa ufugaji nyuki kisasa   "tumejifunza namna sekta hii ya nyuki ilivyo na faida kubwa endapo tutafuga kisasa ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani mazao ya nyuki" ameeleza Bw. Meneja Memuruti Menye. Naye, Mfugaji Bi. Naatosim Parmandi amesema mafunzo ya vitendo yamekua na tija sana, wameweza kutembelea na kushuhudia zoezi la upandishaji na ukaguzi wa mizinga pamoja na uchakataji wa asali unavyofanyika maabara "kabla ya mafunzo nilikuwa natumia njia za kiasili kuvuna asali ambapo zilikua zikiwaathiri nyuki". amesema Parmandi Mtafiti kutoka TAWIRI Bw. Kipemba Ntiniwa ameeleza kuwa, nyuki ni fusra k...

NCAA YASHIRIKI UZINDUZI WA FILAMU YA AMAIZING TANZANIA NA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA KATI YA TANZANIA NA CHINA.

Picha
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeshiriki katika uzinduzi wa filamu ya Amazing Tanzania pamoja na maadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China iliyofanyika tarehe 4 Novemba, 2024 Jijini Dar es Salaam. Katika tukio hilo adhimu na la kihistoria ujumbe wa Tanzania umeongozwa  na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana (Mb) huku ujumbe wa China ukiwakilishwa na Makamu Waziri wa Utalii na Utamaduni Mhe. Lu Yingchuan. Uzinduzi wa filamu ya Amaizing Tanzania na maadhimisho ya miaka 60 ya Kidiplomasia ni hatua muhimu kufuatia juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia, kutangaza na kukuza utalii pamoja na kufungua fursa za uwekezaji kati ya Tanzania na China. Aidha, uzinduzi wa Filamu ya Amazing Tanzania ni jukwaa muhimu katika kutangaza urithi wa kipekee na vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania na kufungua milango zaidi kwa watalii na wawekezaji k...

MBINU MPYA YA KUWADHIBITI TEMBO YAONESHA MWELEKEO WA MAFANIKIO SAME

Picha
Hatimaye mbinu mpya ya kudhibiti changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu hususani tembo iliyobuniwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA ambayo tayari imeanza kutumika kuzuia tembo kuleta athari kwa maisha na mali za wananchi waishio wilaya za Same na Mwanga Mkoani Kilimanjaro imeanza kuonesha mwelekeo wa mafanikio baada ya wananchi kukiri kuwasaidia. Katika nyakati tofauti, wakizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari katika ziara iliyofanywa na TAWA wilaya za Same na Mwanga Oktoba 31, 2024 Mkoani Kilimanjaro wananchi hao wameishukuru TAWA kwa elimu waliyowapa, umoja na ushirikiano wanaoutoa kwao katika kukabaliana na changamoto ya tembo jambo ambalo wanakiri limewasaidia kujilinda dhidi ya madhara yatokanayo na wanyamapori hao na pia kupata mavuno Kwa wakati. "Tunashirikiana na watu wa TAWA vizuri sana na maelekezo wanayotupa kuhusiana na tembo ni mazuri sana, ni kweli hawa tembo wanasumbua lakini Kwa kushirikiana inawezekana kuwakabiri...