📍ASANTENI ARUSHA(WALIMU, WAFANYAKAZI NA SHULE ZOTE ZISIZO ZA SERIKALI MKOA WA ARUSHA


Tunawashukuru walimu na wafanyakazi wa shule za notre dame na canossa kwa kukipokea chama chenu cha TPTU na kujiunga nacho.


Tunalishukuru jimbo kuu katoliki la Arusha, kwa ushirikiano wenu wa dhati kwa chama cha TPTU, kwa kushirikiana nasi na kutuunganisha na shule zenu zote za jimbo kuu la Arusha, ili tuweze kutekeleza takwa la kisheria la kukutana na kuzungumza na kuwasajili uanachama walimu na wafanyakazi wa shule zenu.


Tunawashukuru shule zote zisizo za serikali kwa ujumla wake mkoa wa Arusha, kwa ushirikiano wenu kwa kadri tunavyowafikia mmoja mmoja, shabaha yetu kuu ni kujenga ustawi bora kwa shule zote zisizo za serikali nchini, walimu na wafanyakazi wake wote kwa ujumla wao.


Aidha tunapenda kuwafahamisha kuwa , kwa mkoa wa Arusha, ofisi zetu za chama cha TPTU zinapatikana jengo la NSSF(uzunguni) orofa ya kwanza, chini ya katibu wetu wa chama cha TPTU mkoa wa Arusha, taaluma mwanasheria, Bi Aika kweka, simu 0763143442 na 0784719109, tunawakaribisha sana ofisini kwetu kwa ufafanuzi zaidi kuhusu TPTU na huduma zetu zingine mbalimbali, ikiwemo huduma za wadau wote tunaoshirikiana nao.






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE