Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2024

BUSHMAN SAFARI TRACKERS YATOA MSAADA WA PIKIPIKI 6 KWA ASKARI WA TAWA

Picha
Katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika ulinzi wa rasilimali za wanyamapori nchini, Kampuni ya Bushman Safari Trackers iliyopo Mkoani Morogoro imetoa msaada wa pikipiki sita (6) zenye thamani ya shilingi za kitanzania Millioni Kumi na tano (15,000,000) Kwa Askari wa Uhifadhi wa TAWA kwa ajili ya kusaidia shughuli za doria katika Pori la Akiba Maswa. Akimkabidhi Kaimu Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Mlage Kabange msaada huo katika Ofisi za Makao Makuu ya TAWA zilizopo Mkoani Morogoro Oktoba 31,2024, Captain Willness Minja kwa niaba ya Kampuni ya Bushman amesema wamekabidhi vitendea kazi hivyo kwa ajili ya kusaidia shughuli za doria katika Pori la Akiba Maswa wao kama miongoni mwa wadau wakubwa wa uhifadhi katika hifadhi hiyo. Kwa upande wake, Kaimu Naibu Kamishna Kabange ameishukuru Kampuni ya Bushman kwa ufadhili huo ambao unalenga kuimarisha usimamizi wa shughuli za uhifadhi na ulinzi wa rasilimali za wanyamapori. "Tunashukuru sana wawekezaji wetu kwa msaada huu na vitendea ...

TANZANIA MBIONI KUZALISHAJI MADINI YA NIOBIUM

Picha
Imeelezwa kwamba Tanzania ipo mbioni kuanza uzalishaji wa madini ya Niobium ambayo ni moja ya madini adimu yanayotumika katika mitambo mbalimbali ikiwemo matumizi ya  utengenezaji wa  injini za Ndege na Roketi. Hayo yamesemwa leo Bungeni  na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa  wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa jimbo la Mbeya Vijijini Mhe. Oran Njema kuwa ni lini uzalishaji wa madini ya Niobium na kiwanda cha uzalishaji wa Ferroniobium utaanza katika Halashauri ya Wilaya ya Mbeya.  Dkt. Kiruswa amesema kuwa, mradi wa uchimbaji wa madini ya Niobium katika eneo la Panda Hill unamilikiwa na kampuni ya Panda Hill Tanzania Limited (PHTL) kwa ajili ya uzalishaji wa mazao yanayotokana na madini hayo ikiwemo zao la madini ya ferroniobium linalotokana na uchakataji wa madini ya Niobium. Aidha, Dkt. Kiruswa ameongeza kuwa, tayari Serikali imeanza majadiliano na kampuni ya Panda Hill kwa lengo la kusaini Mkataba wa Makubaliano utakaowezesha Serikali kup...

DCEA KANDA YA KASKAZINI YAHAMASISHA UMMA KUPIGA VITA DAWA ZA KULEVYA KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NOVEMBA 27 2024

Picha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 23.10.2024 imetoa elimu juu ya madhara ya kuchagua kiongozi wa Serikali za Mitaa anayejihusisha na rushwa pamoja na matumizi au biashara haramu ya dawa za kulevya katika kipindi cha Kurunzi kinachorushwa mbashara katika redio ya kijamii iitwayo Redio 5 FM iliyopo Njiro jijini Arusha.  Aidha, elimu hiyo iliambatana na kuelezea mafanikio ya mwaka mmoja katika shughuli za operesheni na uelimishaji tangu kuanzishwa Ofisi ya Mamlaka Kanda ya Kaskazini yenye makao makuu yake jijini Arusha.  Pia, wasikilizaji wa redio hiyo walihamasishwa kupiga namba ya simu ya bure ya 119 kwaajili ya kutoa taarifa ya wahalifu wa dawa za kulevya katika mitaa yao wanayoishi. 

TUZO YA USIKU WA MADINI 2023 YAMPA HAMASA KUANZISHA KAMPUNI

Picha
Tuzo ya Mwanamke Bora katika Sekta ya Madini Mwaka 2023 ilikwenda kwa Mwanadada Leminatha Cornel Kabigumila mama wa Watoto wawili mwenye umri wa miaka 38. Kabla ya kushinda tuzo hiyo, Leminatha alikuwa akimiliki jumla ya leseni 4 za uchimbaji mdogo wa madini ya Bati (Tin)  Tuzo hiyo ilimpa hamasa kubwa ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini na sasa ameanzisha kampuni inayojulikana kama Rare Mining East Africa LTD yenye jumla ya leseni 21 za uchimbaji mdogo wa Madini ya bati na leseni 74 zipo kwa jina lake.  Ili kupata leseni hizo, ilimlazimu Bi. Leminatha kulipa kiasi cha shilingi milioni 150 Serikalini ikiwa ni ada za leseni baada ya wamiliki wa awali kushindwa kuzilipia na kuziendeleza. Pia, alilipia leseni 33 za mdaiwa mwingine kwa kiasi cha shilingi milioni 120 na kuziendeleza. Kwa kifupi ni kwamba hivi sasa mwanamama huyu anamiliki jumla ya leseni 95 za uchimbaji mdogo wa madini ya bati (Tin) na 1 ya dhahabu zote zikiwa hai na zinaendelezwa. ‘’ Ile tuzo ilinipa hamasa kubwa n...

TAWA YAWASILISHA TAARIFA YA UTENDAJI WAKE KWA KAMATI YA BUNGE

Picha
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA leo Oktoba 24, 2024 katika ukumbi  namba 44 jengo dogo la utawala bungeni Dodoma imewasilisha taarifa ya utendaji wake ya mwaka 2023/24 kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii iliyojikita katika kudadavua majukumu ya kiuhifadhi na utalii katika kipindi husika. Akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) Kwa niaba ya Kamishna wa uhifadhi wa TAWA, Kaimu Naibu Kamishna wa Uhifadhi Mlage Kabange amesema katika kipindi cha mwaka 2024/25, Mamlaka imepanga kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi billioni 94 ambapo hadi kufikia mwezi Septemba, 2024 Mamlaka imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 23.8 sawa na asilimia 102.96 ya lengo la robo ya kwanza ya mwaka. Kuhusu ongezeko la matukio ya wanyamapori wakali na waharibifu nchini Kabange amesema Wizara imekuja na mkakati wa kuvuna baadhi ya spishi za wanyamapori hao ili kupunguza athari Kwa maisha ya wananchi na mali zao ambapo amebainis...

MSAJILI WA HAZINA AIPONGEZA TAWIRI,AHIMIZA UBUNIFU KATIKA KUJIENDESHA

Picha
Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kwa shughuli za utafiti wa Wanyamapori ambazo zina tija katika sekta ya uhifadhi na utalii ambayo inachangia asilimia 17% ya pato la Taifa. Akizungumza jijini Arusha wakati wa kikao na Menejimenti ya TAWIRI, Bw. Mchechu amesema Ofisi ya msajili wa Hazina itaendelea kushauri vyema katika kuimarisha Mashirika ya Umma yaweze kujiendesha kwa tija.   “nawapongeza kwa utendaji mzuri, nitoe wito kuendelea kuwa wabunifu kutumia rasimali mlizo nazo kujiendesha kwa ufanisi” amehimiza Bw.Mchechu Naye, Mkurugenzi Mkuu TAWIRI Dkt, Eblate Mjingo amesema TAWIRI ni taasisi ya kimkakati ambayo mbali na kutokuonekana ikizalisha fedha moja kwa moja ina mchango mkubwa katika mapato yatokanayo na utalii nchini ambapo takwimu na taarifa za tafiti ndizo zinazonadi utalii na kuimarisha uhifadhi

TAZAMA PICHA 10 GARI LAPARAMIA MGHAHAWA WA CAFE LA ZAYN NI BAADA YA DEREVA WA GARI HILO KUNYIMWA SUKARI ,WATEJA WATIMUA MBIO BAADHI WATERUHIWA VITUMBUA VYAZAGAA

Picha
TAHARUKI imewakumba wateja katika mgahawa maarufu wa CAFE LA ZAYN jijini ARUSHA, baada ya gari kuparamia mghahawa huo wakinywa chai na kufanya uharibifu mkubwa huku baadhi ya wateja wakijeruhiwa kwa kukatwa na vioo. Tukio hilo lakushtua limetokea mapema leo jumamosi Agosti 19,mwaka huu, katika mghahawa huo uliopo eneo maarufu la ROUND ABOUT ya Florida , majira ya asubuhi wakati gari hilo aina yaToyota LAND CRUISER lenye namba T 244 CML kuparamia mgahawa huo wakati wateja wakiendelea kunywa chai na kuwalazimu kutimua mbio kwa lengo la kujinusuru huku baadhi yao kujeruhiwa na kukimbizwa hospitali . Baadhi ya shuhuda wamedai kwamba dereva wa gari hilo ambaye hakufahamika mara moja jina lake alikuwa akinywa chai katika mghahawa huo na aliomba kupatiwa sukari, lakini ghafla alitoweka na kwenda kwenye gari hilo . Walisema dereva huyo aliingia kwenye gari na kuliondoa kwa kasi akirudi nyuma na kugonga gari jingine lililokuwa linapita barabarani ,baadaye alianza kuondoka kwa kasi kwenda ...

BINGWA WA MAGONJWA YA SARATANI KUTOKA HOSPITALI YA HCG IPO ARUSHA SASA

Picha
  Habari njema kwa wakazi wote wa Arusha, Daktari bingwa wa magonjwa ya saratani kutoka hospitali ya HCG ya nchini India anakuja jijini Arusha kwenye kambi ya siku 2 ya magonjwa ya saratani, itakayoratibiwa na MedINCREDI kwa kushirikiana na hospitali ya NSK Hospitals Kambi hii itakayofanyika kati ya tarehe 24/10/2024 kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni,na tarehe 25/10/2024 kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana, itatoa nafasi ya wagonjwa wote wanaosumbuliwa na magonjwa ya saratani, kumuona daktari huyu bingwa kwa gharama ya shilingi 35,000/- tu. Kwa mawasiliano zaidi  0626 221 331 0786 524 323 0782 410 548

POLISI WAONYA MADEREVA:MWENDOKASI NA ULEVI VYATAJWA KUSABABISHA AJALI NYINGI

Picha
Moshi. Mwendokasi umetajwa kuwa chanzo kikubwa cha ajali nyingi barabarani nchini, huku madereva wakionywa kuhusu matumizi ya vilevi na kutokuzingatia alama za barabarani.  Hayo yameelezwa leo alfajiri, Oktoba 17, 2024, na Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma na Mafunzo kutoka Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Michael Deleli, alipokuwa akizungumza na madereva katika Kituo Kikuu cha Mabasi Moshi, mkoani Kilimanjaro. ACP Deleli amebainisha kuwa asilimia kubwa ya ajali barabarani zinasababishwa na makosa ya kibinadamu, akiwataka madereva kuendesha kwa uangalifu ili kuepusha ajali zinazogharimu maisha ya watu na Taifa kwa ujumla.  "Baadhi ya madereva wanatumia vilevi na kushindwa kuzingatia sheria za usalama barabarani, hali inayochangia ajali nyingi. Tunafanya zoezi la kupima ulevi kwa madereva ili kudhibiti hali hii," alisema ACP Deleli. Aidha, aliwasisitiza madereva kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa abiria wao ili kujenga uaminifu ...

DCEA YATOA ELIMU KINGA DHIDI YA TATIZO LA DAWA ZA KULEVYA WILAYANI LONGIDO ARUSHA

Picha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini  kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Longido tarehe 15.10.2024 imetoa elimu kinga dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa wanafunzi 405 wa Shule ya Msingi Namanga na Wanafunzi 803 wa Shule ya Sekondari ya Namanga katika eneo la mpaka, Kata ya Namanga wilayani Longido Arusha (M). Wanafunzi hao walihamasishwa wakatae dawa za kulevya ili waweze kutimiza ndoto zao za kielimu.  Pia, walihimizwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kwa kupiga namba ya simu ya bure ya 119.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII AFANYA ZIARA YA KIKAZI TAWIRI

Picha
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana(Mb) amefanya ziara katika makao makuu ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Njiro - Arusha, ambapo amebainisha umuhimu wa Tafiti za Wanyamapori katika kupata takwimu za Kisayansi zinazotumika kufanya maamuzi. Akizungumza katika kikao na Menejimenti ya TAWIRI Mhe. Chana amesema Serikali inatumia takwimu za kisayansi kufanya maamuzi yaliyojikita kuimarisha uhifadhi wa Wanyamapori ili kuwa na Utalii endelevu. " Tunahakikisha rasilimali hii ya Wanyamapori ipo kwa kizazi cha leo na kijacho ambapo matumizi ya takwimu za kisayansi ni dira katika uhifadhi amesisitiza Waziri Chana. Mkurugenzi Mkuu TAWIRI Dkt.Eblate Mjingo amesema takwimu za tafiti zinasaidia kunadi Utalii ikiwa ni pamoja na kuelekeza namna bora ya kufanya Utalii sambamba na kuimarisha uhifadhi. Aidha, Pamoja na mambo mengine Waziri Chana amepokea taarifa mbalimbali za utendaji kazi wa Taasisi hiyo. Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katib...

LEMA ASHUSHA SHUTUMA NZITO KWA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI ARUSHA,KAYOMBO AJIBU CHAP KWA FACT "HAO CHADEMA SIJAWAONA KWANGU WAKIJA KULALAMIKA NA MIMI SIWEZI KUWAPIGIA SIMU"

Picha
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, John Kayombo, ameibuka na majibu makali kufuatia madai yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, kuhusu dosari kadhaa katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwenye daftari la mkazi linaloendelea nchini. Jana jumatatu  Lema akizungumza  na vyombo vya habari jijini  hapa,alimshambulia vikali Mkurugenzi wa jiji la Arusha,John Kayombo akidai anatumika vibaya na ccm akidai ni mpango maalumu ulioandaliwa kumleta Arusha ili kuisaidia ccm kushinda katika uchaguzi huo jambo ambalo alisema amejipanga  kula naye sahani moja labda ahamishwe. " Watu wanasombwa kwa magari ya Haice kutoka kata moja kwenda kata nyingine kujiandikisha maana yake nini hii ni hujuma inayofanywa na msimamizi wa uchaguzi kwa kushirikiana  na ccm"Alisema Lema!  Akizungumza ofisini kwake Kayombo ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi huo, amekanusha vikali madai ya Lema, akisisitiza kuwa zoezi la uandikishaji linaendele...

HAMASA YATOLEWA KWA WACHIMBAJI WA MADANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA MPIGA KURA GEITA

Picha
Mwenyekiti wa chama cha Wachimbaji wadogo Mkoa wa Geita (GEREMA) Titus Kabuo na mwekezaji katika sekta ya madini mkoani Geita Titus Kabuo ameonyesha mfano kama kiongozi kwa kuchukua hatua ya kipekee ya kuingia ndani ya maduara yenye urefu wa mita 400 chini ya ardhi kwenye migodi yake ya dhahabu.  Kabuo, alichukua hatua hiyo ili kuhamasisha wafanyakazi wake kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura Hatua hiyo inalenga kuwapa wafanyakazi wake nafasi ya kushiriki kikamilifu katika michakato ya kidemokrasia ya nchi yao, jambo linaloweza kuleta mabadiliko chanya kwa jamii na taifa kwa ujumla. Akizungumza na waandishi wa habari alioambatana naye kwa wafanyakazi wa mgodi huo, Kabuo alisisitiza umuhimu wa kila raia kutumia haki yake ya kidemokrasia kwa kujiandikisha kupiga kura.  "Sisi sote tuna wajibu wa kuhakikisha kuwa sauti zetu zinasikika katika masuala muhimu ya kitaifa, na njia pekee ya kufanya hivyo ni kwa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi hakikisheni mnawahi katika v...

ETDCO KUJENGA MIUNDO MBINU YA UMEME MIGODINI

Picha
Kampuni Tanzu ya Umeme Tanesco (Etdco) inayojishughulisha na Ukarabati wa miundombinu ya Umeme katika maeneo mbalimbali  imefanikiwa kujenga miundo mbinu na viunganishi vya migodi ya umeme nchini Tanzania. Katika mahojiano na waandishi wa habari kwe Viwanja vya bombambili Mkoani Geita kwenye maonesho ya saba (7) ya Teknolojia ya madini Kaimu Mkurugenzi Huduma Za Ufundi wa kampuni ya Etdco mhandisi Dismas Massawe amesema kuwa kampuni hiyo ni kampuni inayomilikiwa na Serikali yaani Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa asilimia mia moja 100%. Amesema mpaka sasa wamefanikiwa kujenga miundo mbinu kadhaa ya umeme,kujenga laini ya kilomita 100 kutoka Geita mpaka eneo la StamiGold ( Stamico ) na kuunganishia umeme. Amesema, pia wamefanikiwa kujenga mradi mwingine wa kuunganishia umeme Mgodi wa GeitaGold mine (GGML) ,kujenga kilomita 58 kuunganisha umeme katika mgodi wa Kabanga nikel Ngara. mhandisi Dismas Massawe amesema kwa sasa wanaendelea na ujenzi wa line kule Katavi,kuunganisha ume...

TAZAMA PICHA TUKIO LA MAUAJI YA MWANAFUNZI ARUSHA,WANANDOA WADAIWA KUMCHINJA KAMA KUKU NA KUMKATAKATA VIPANDE NA KUMFICHA UVUNGUNI AKIWA KWENYE BESENI ,MKE NI 'SWALA TANO BALAA',YAKUTWA ORODHA NDEFU WALIOUAWA,WANANCHI WABOMOA NYUMBA YAKE

Picha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia wanandoa wawili ,Jaina Mchomvu(50) na Ramji Hatibu Mlacha(60) wakituhumiwa kumuua kwa kumchinja mwanafunzi wa darasa la Sita wa shule ya Msingi Domino, Mariam Juma(12) mkazi wa kwa Mrombo katika jiji la Arusha Tukio hilo la kusikitisha linalohusishwa na imani za ushirikina,mwili wa marehemu ulikutwa mchana saa sita chini ya uvungu wa kitanda ukiwa umekatwakatwa vipande na kuwekwa kwenye beseni baada ya mjukuu wa mtuhumiwa kuona mkono wa marehemu ukining'inia wakati akitafuta kiatu .                                        Rpc Masejo Mama wa Marehemu   Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Justine Masejo amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa  mtoto huyo kabla ya kifo chake  alikuwa ametumwa dukani toka asubuhi lakini hakurejea na ilipofika mchana wazazi wake walianza kumtafuta maeneo mbalimbali baada ya kuingiwa na wasiwasi. Kamanda Mas...