DCEA KANDA YA KASKAZINI YAHAMASISHA UMMA KUPIGA VITA DAWA ZA KULEVYA KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NOVEMBA 27 2024
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 23.10.2024 imetoa elimu juu ya madhara ya kuchagua kiongozi wa Serikali za Mitaa anayejihusisha na rushwa pamoja na matumizi au biashara haramu ya dawa za kulevya katika kipindi cha Kurunzi kinachorushwa mbashara katika redio ya kijamii iitwayo Redio 5 FM iliyopo Njiro jijini Arusha.
Aidha, elimu hiyo iliambatana na kuelezea mafanikio ya mwaka mmoja katika shughuli za operesheni na uelimishaji tangu kuanzishwa Ofisi ya Mamlaka Kanda ya Kaskazini yenye makao makuu yake jijini Arusha.
Pia, wasikilizaji wa redio hiyo walihamasishwa kupiga namba ya simu ya bure ya 119 kwaajili ya kutoa taarifa ya wahalifu wa dawa za kulevya katika mitaa yao wanayoishi.

Maoni
Chapisha Maoni