Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2026

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

Picha
Katika maombi hayo namba 83/2025 yalifunguliwa na Chemli Mallya dhidi ya Anna Mallya (ambaye ni shemeji yake),mgogoro unaotajwa kuwepo kwa zaidi ya miaka 10 tangu mume wa Anna ambaye ni kaka wa Chemli, Mathias Mallya,aliyefariki mwaka 2010 Moshi.Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Moshi limelifuta shauri la ardhi linalowahusisha wanaukoo wa Mallya baada ya kubaini kuwa mleta maombi alikiuka amri ya awali ya marekebisho ya hati ya maombi. Uamuzi huo umetolewa Februari 24,2026 na Mwenyekiti wa Baraza hilo,Hussen Lukeha, baada ya kukubaliana na pingamizi la awali lililowasilishwa na mjibu maombi. Shauri hilo la maombi namba 83/2025 lilifunguliwa na Chemli Mallya ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Sisamaro, Kata ya Kibosho Okaoni,Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro,mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 10. Mjibu maombi katika shauri hilo ni Anna Midimito, mjane wa marehemu Mathias Mallya aliyefariki mwaka 2010, ambaye alikuwa mdogo wa mleta maombi,Chemli Mallya. Akitoa uamuzi huo Mwenyekiti hu...

ASKARI KUTOKA TANZANIA WAVISHWA NISHANI KUTAMBUA MCHANGO WA KULINDA AMANI SUDANI KUSINI..

Picha
Maafisa,na askari wa vyeo mbalimbali kutoka Jeshi la Polisi Nchini Tanzania ambao nikundi lilomaliza muda wake wa kuhudum kulinda amani nchini Sudan kusini wamehitimisha kwa Paredi maalum ambayo ili ambatana na kuwavisha nishani( Medall Pin) maafisa na askari hao ikiwatambua kwa kazi nzuri ya kudumisha amani. Tanzania ni miongoni mwa nchi bora zinazochangia askari wake katika Operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa. Aidha Miongoni mwa maafisa hao wamebainisha kuwa licha ya kuwa mazingira magumu ya iliwapa moyo kuendelea kulinda amani na kutoa elimu kwa makundi mengi zaidi. Sambamba na hilo wameendelea kuwashukuru maafisa wengine wa majeshi kwa namna walivyoshirikiana kudumisha amani katika misheni ya kulinda amani nchini Sudan Kusini Mwisho wamewaomba wananchi wa Sudan kusini kuendelea kutunza na kulinda amani ya nchini hiyo

ZARA TOURS YANG'ARA TENA KWENYE TUZO ZA SERENGETI, NA KUPANUA MFUMO WAKE WA HESHIMA ZA KIMATAIFA

Picha
Kampuni ya utalii ya Zara Tours ya mjini Moshi kwa mara nyingine imethibitisha uongozi wake katika sekta ya utalii nchini Tanzania baada ya kujinyakulia tuzo nyingine ya heshima kwenye tuzo za Serengeti, na kuendeleza msururu wa heshima ambao kampuni hiyo imekuwa ikijipatia karibu kila mwaka.  Tuzo hiyo ni miongoni mwa tuzo 51 zilizotolewa wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za Serengeti iliyofanyika usiku wa kuamkia jana kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha, hafla iliyowakutanisha wadau wakuu wa utalii kutoka Tanzania na nje ya nchi.   Naye Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha Dkt.Mwigulu Nchemba ameipongeza sekta ya utalii kwa mchango wake mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa, kutengeneza fursa za ajira na kuitangaza Tanzania duniani. Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Zara Tours, Bi. Zainabu Ansell alisema mafanikio hayo yanadhihirisha uchapakazi, ari ya pamoja na ushirikiano wa karibu kati ya serikali na wadau wa sekta binafsi hususan katika ulinzi na...