DCEA YATOA ELIMU KINGA DHIDI YA TATIZO LA DAWA ZA KULEVYA WILAYANI LONGIDO ARUSHA


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini  kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Longido tarehe 15.10.2024 imetoa elimu kinga dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa wanafunzi 405 wa Shule ya Msingi Namanga na Wanafunzi 803 wa Shule ya Sekondari ya Namanga katika eneo la mpaka, Kata ya Namanga wilayani Longido Arusha (M).


Wanafunzi hao walihamasishwa wakatae dawa za kulevya ili waweze kutimiza ndoto zao za kielimu. 


Pia, walihimizwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kwa kupiga namba ya simu ya bure ya 119.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE