MSAJILI WA HAZINA AIPONGEZA TAWIRI,AHIMIZA UBUNIFU KATIKA KUJIENDESHA


Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kwa shughuli za utafiti wa Wanyamapori ambazo zina tija katika sekta ya uhifadhi na utalii ambayo inachangia asilimia 17% ya pato la Taifa.


Akizungumza jijini Arusha wakati wa kikao na Menejimenti ya TAWIRI, Bw. Mchechu amesema Ofisi ya msajili wa Hazina itaendelea kushauri vyema katika kuimarisha Mashirika ya Umma yaweze kujiendesha kwa tija.

 

“nawapongeza kwa utendaji mzuri, nitoe wito kuendelea kuwa wabunifu kutumia rasimali mlizo nazo kujiendesha kwa ufanisi” amehimiza Bw.Mchechu


Naye, Mkurugenzi Mkuu TAWIRI Dkt, Eblate Mjingo amesema TAWIRI ni taasisi ya kimkakati ambayo mbali na kutokuonekana ikizalisha fedha moja kwa moja ina mchango mkubwa katika mapato yatokanayo na utalii nchini ambapo takwimu na taarifa za tafiti ndizo zinazonadi utalii na kuimarisha uhifadhi




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE