DCEA YATOA ELIMU KINGA JUU YA MADHARA YA TATIZO LA DAWA ZA KULEVYA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA TURKISH MAARIF JIJINI ARUSHA


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Asasi ya Youth and Community Rehabilitation (YCR) na Drug Abuse and Recovery Organization (DARO) tarehe 25.09.2024 imetoa elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya katika shule ya sekondari Turkish Maarif iliyopo Ngaramtoni Arumeru (W) Arusha (M).


Aidha, elimu hiyo ilitolewa kwa wanafunzi zaidi ya 230 ikiwa na lengo la kuwapa elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya pamoja na kuwapa mbinu wanazopaswa kuzitumia ili waweze kujikinga na matumizi ya dawa za kulevya.


Ofisi ya Mamlaka Kanda ya Kaskazini itaendelea kushirikiana na Asasi za Kiraia katika utekelezaji wa majukumu yake kwa lengo la kuwawezesha na kuimarisha mashirikiano ambayo tunaamini yatasaidia kueneza elimu zaidi kwa jamii ili tuweze kupata matokeo yenye tija zaidi.





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE