𝐌𝐖𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐘𝐀𝐍𝐆’𝐀𝐑𝐀: 𝐓𝐀𝐍𝐀𝐏𝐀 𝐘𝐀𝐙𝐈𝐍𝐃𝐔𝐀 𝐊𝐀𝐌𝐏𝐄𝐍𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀 “𝐕𝐀𝐋𝐄𝐍𝐓𝐈𝐍𝐄 𝐖𝐄𝐄𝐊𝐄𝐍𝐃 𝐆𝐀𝐓𝐄𝐀𝐖𝐀𝐘 𝐍𝐀 𝐓𝐀𝐍𝐀𝐏𝐀” 𝐍𝐃𝐀𝐍𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐈𝐖𝐀 𝐂𝐇𝐀 𝐒𝐀𝐀𝐍𝐀𝐍𝐄


Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa kushirikiana na Kampuni ya @busybee_cabins imezindua Kampeni yake ijulikanayo Valentine Weekend Gateway na TANAPA jana Januari 21, 2025 jijini Mwanza, lengo likiwa ni kuhamasisha Watanzania na wasio Watanzania kutembelea Hifadhi za Taifa kipindi hiki cha msimu wa Sikukuu ya Wapendanao.


Akizungumzia dhima ya uzinduzi wa kampeni ya Valentine Weekend Gateaway na TANAPA, Kamishna Lyimo alisema, “Leo tunazindua kampeni hii kwa Hifadhi zote 21, tunawahamasisha Watanzania wote watembelee Hifadhi zetu maana tumeandaa vifurushi rafiki vya bei nafuu vinavyomwezesha kila Mtanzania kumudu gharama za kutalii msimu wa wapendanao.”


Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Dr. Tutindaga Mwakijambile, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane, alitoa maelezo kuhusu Kisiwa cha Saanane ambapo ni mahali pa kipekee kwa wapendanao. Mandhari tulivu, fursa za kipekee za kupumzika, na shughuli mbalimbali za kuburudisha zinazotengeneza uzoefu wa kukumbukwa milele.


Kamishna Dr. Tutindaga alisema “tumejiandaa kuwahudumia wapendanao, Watalii wataweza kutembelea Kisiwa cha Saanane chenye msitu wa kijani uliosheheni miamba minene ya mawe iliyobanana, wanyama kama Swala, Nyumbu, Simba, Mamba, na Ndege wa aina mbalimbali pamoja na mandhari nzuri ya jiji la Mwanza.”


Mkurugenzi wa Kampuni ya Busybee, Baraka Nyororo, alieleza kwa upana kuhusu ushirikiano na TANAPA katika kuandaa tukio hilo adhimu katika jiji la Mwanza, ambapo Watanzania wengi wanatarajiwa kushiriki kutembelea kisiwa hicho siku ya Februari 15, 2025


TANAPA imeendelea kunadi na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika Hifadhi za Taifa nchini hasa kupitia matukio ambayo yamepelekea kupatikana kwa mafanikio makubwa katika sekta ya Utalii.








Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE