_*DCEA YATOA ELIMU KATIKA ENEO LA MIGODI LA MUNDARARA ARUSHA*_


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 17.01.2025 imetoa elimu kwa wananchi na wachimba madini zaidi ya 95 katika eneo la migodi ya madini aina ya rubi Mundarara wilayani Longido Arusha (M).


Washiriki wa elimu hiyo walitolewa dhana potofu kuwa dawa za kulevya husababisha kupata madini mengi, bali walielimishwa kuwa dawa za kulevya zinasababisha madhara ya kiafya, kijamii na kiuchumi. 


Katika mkutano huo wananchi na wachimba madini hao walihamasishwa kushirikiana na Mamlaka katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kupitia namba ya simu ya bure ya 119.







*MWISHO*

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE