DCEA YAHITIMISHA MAFUNZO YA KIMATAIFA KATIKA KUWAJENGEA UWEZO ASASI ZA KIRAIA JIJINI ARUSHA*


DCEA yazijengea uwezo Asasi za Kiraia Arusha kwa kuwapa miongozo sahihi ya uelimishaji umma ngazi ya familia_*

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Taasisi ya Colombo Plan Drug Advisory Programme (CP-DAP) tarehe 22.05.2025 imehitimisha mafunzo maalum ya siku 5 ya kuwajengea uwezo Asasi za Kiraia juu ya Mtaala wa Kimataifa wa utoaji elimu kinga sahihi dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa ngazi ya familia (Universal Prevention Curriculum-UPC Family Based Prevention) kwa Wawakilishi wa Asasi za Kiraia 24 katika Ukumbi wa YCR uliopo Ngarenaro jijini Arusha. 


Mafunzo hayo ya siku tano yamewaweza washiriki hao kupata mbinu mpya zilizothibitishwa kisayansi zitakazowasaidia katika kutoa elimu kinga ngazi ya familia. 



Aidha, washiriki wa mafunzo hayo walipatiwa vyeti vinavyotambulika kimataifa katika utoaji elimu sahihi dhidi ya tatizo la dawa za kulevya. Hivyo, wataalamu hao wataenda kuisaidia jamii ya kitanzania katika kuondoa tatizo la dawa za kulevya katika familia.


*_DCEA Kanda ya Kaskazini itaendelea kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wanaofanya kazi ya udhibiti wa dawa za kulevya zikiwemo Asasi za Kiraia ili kuhakikisha malengo ya Serikali katika kutoa elimu sahihi juu ya madhara za dawa za kulevya yanafikiwa._*





*_MWISHO_*

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE