*WAZIRI MKUU AWASILI ARUSHA KWA ZIARA YA SIKU MOJA*
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba leo Jumapili Novemba 30, 2025, amewasili Mkoani Arusha kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wa Serikali, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu.
Mhe. Waziri Mkuu anafanya ziara ya Kikazi ya siku moja Mkoani Arusha ambapo pamoja na mambo mengine, anatarajiwa kuwa na Mkutano mkubwa wa hadhara kwenye Viwanja vya Magufuli, Leganga, Kata ya Usa River, Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.




Maoni
Chapisha Maoni