MSIMAMIZI WA UCHAGUZI ARUSHA MJINI: WALIOPOTEZA KADI YA KURA WATARUHUSIWA KUTUMIA NIDA, LESENI AU PASI YA KUSAFIRI.


Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Arusha Mjini ametangaza rasmi kuwa Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika siku ya Jumatano, tarehe 29 Oktoba 2025, kwa mujibu wa Kifungu cha 69(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024.




Kwa mujibu wa tangazo hilo, vituo vilivyotumika kuandikisha wapiga kura ndivyo vitakavyotumika kupigia kura siku ya uchaguzi. Vituo hivyo vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi (2:00) na kufungwa saa 10:00 jioni (10:00).

Aidha, kwa wapiga kura wa magereza, vituo vyao vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi (2:00) na kufungwa saa 9:00 alasiri (9:00).

Taarifa Muhimu kwa Wananchi

Sambamba na tangazo hilo, kwa kila kituo cha kupigia kura zimebandikwa taarifa zifuatazo:

Mfano wa karatasi ya kura yenye majina, picha, na nembo za vyama vya wagombea wa nafasi za Rais, Wabunge na Madiwani;
Orodha ya majina ya wapiga kura walioandikishwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi;
Orodha ya wapiga kura waliopangiwa kupiga kura ya Rais pekee.


Wananchi wote wanahimizwa kupitia taarifa hizo mapema ili kutambua vituo vyao vya kupigia kura na kujiridhisha na majina yao kwenye orodha.


Utambulisho wa Mpiga Kura.


Siku ya uchaguzi, kila mpiga kura anatakiwa kufika kituoni na kadi yake ya mpiga kura.

Hata hivyo, kwa wale waliopoteza kadi zao lakini waliosajiliwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, wataruhusiwa kupiga kura endapo watakuwa na kitambulisho mbadala kama:

Leseni ya udereva,
Pasi ya kusafiria, au
Kitambulisho cha Taifa (NIDA).

Ni muhimu majina yaliyomo kwenye kitambulisho mbadala yawe yanalingana na yaliyoko kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.






Wito kwa Wananchi



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE