RC MAKONDA AMEWAAGIZA MADIWA WA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA WAKAMILISHE MIRADI YOTE


MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewaagiza madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kuhakikisha wanakamilisha miradi yote ya viporo ikiwemo ujenzi wa barabara, soko na stendi ya kisasa.


Makonda ameyasema hayo katika kikao cha Baraza Maalum la Madiwani la kupitisha bajeti ya Sh bilioni 119 huku makusanyo ya mapato ya ndani yakiwa ni Sh milioni 51.2 kwa mwaka 2025/2026.


“Haiwezekani miradi inapoanza maneno yanakuwa mengi ilhali wananchi wanahitaji maendeleo hakikisheni miradi yote viporo ikamilishwe kwa wakati lakini pia pandeni miti msipande fitna,”amesema Makonda.

RC Makonda amesema anataka mkoa huo kuwa namba moja kwa kila kitu na kwamba hawatokubali mkoa huo kupunguza mapato waliyojiwekea bali mapato yaongezeke ikiwemo kila diwani kuhakikisha maendeleo katika kata yake yanakuwa ikiwemo miradi ya maendeleo


Wakati huo huo, Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha wamemwomba RC Makonda kuchukua fomu ya kugombea ubunge mwaka 2025 ili kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa ajili ya utatuzi wa kero mbalimbali za wananchi ikiwemo miradi ya maendeleo.




Naibu Meya wa Jiji hilo, Abrahim Mollel ambaye ni Diwani wa Kata ya Kimandolu kwa kwaniaba ya madiwani wa jiji hilo wakati wa kikao cha baraza hilo amesema: “Ikipendeza kipenga kikiita RC Makonda achukue fomu ya kuwania ubunge kwa jimbo hilo sababu ni kiongozi wa mfano anayeleta mabadiliko chanya kwa wananchi mbalimbali sanjaro na kutatua kero zao”.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE