DCEA YATOA ELIMU KWA WALIMU WAKUU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ZA JIJI LA ARUSHA
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 25.02.2025 imetoa elimu juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya kwa walimu wakuu zaidi ya 200 wa Shule za Msingi na Sekondari za Jiji la Arusha katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Kijenge.
Walimu hao walielezewa uhusiano uliopo kati ya tatizo la dawa za kulevya na changamoto ya afya ya akili, kuwa matumizi ya dawa za kulevya huamsha magonjwa ya akili. Pia walikumbushwa wajibu wao kama walimu wakuu wa kusimamia programu mbalimbali za kuondoa tatizo la dawa za kulevya na afya ya akili shuleni kwao.
Walimu hao walisisitizwa kuendelea kushirikiana na Mamlaka kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kupitia namba ya simu ya bure ya 119




Maoni
Chapisha Maoni