SERIKALI YAKOSHWA MAANDALIZI KABAMBE SIKU YA WANAWAKE ARUSHA.

 


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na makundi maalum Dkt. Doroth Gwajima amefika Mkoani Arusha na kukagua maandalizi ya Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, ambayo kitaifa yatafanyika Mkoani Arusha, akiridhishwa na maandalizi mazuri na kutangaza kuwa Kiwango cha maandalizi yanayofanywa Mkoani Arusha kitakuwa kiwango cha kutolewa mfano kwenye maadhimisho yajayo.


Waziri Gwajima aliyeambatana na washauri wa Rais Mhe. Sophia Mjema na Mhe. Angellah Kairuki, wakati akizungumza na Kamati za maandalizi ya maadhimisho hayo Jijini Arusha, ameagiza kuandaliwa kwa Kamati ndogo itakayoangazia maandalizi ya maadhimisho hayo ngazi ya Mkoa na kuahidi kutangaza Mikoa iliyofanya vizuri mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, anayetarajiwa kuwa Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo kwa mwaka huu.


"Mikoa ipo mingi na mimi nilijiuliza Arusha mmepataje hii fursa, Kumbe ndiyo mambo yenu haya? Arusha hamna jambo dogo, mmefunika kwa maandalizi yenu, wamejiandaa kote ila ninyi ni namba moja. Standard (Kiwango) cha maandalizi mlichokifanya ndiyo tutakayolinganisha na mikoa mingine." Amesema Waziri Gwajima.


Maadhimisho ya kitaifa ya siku ya wanawake duniani yatafanyika Machi 08, 2025,Jijini Arusha kwenye viwanja vya michezo vya Sheikh Amri Abeid Karume, Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ambapo kabla ya kilele chake kwa wiki nzima kutafanyika shughuli mbalimbali Mkoani humo ikiwa ni pamoja na elimu mbalimbali, msaada wa kisheria pamoja na mashindano ya michezo mbalimbali ikiwemo ya magari itakayohusisha wanawake.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE