MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA APOKELEWA NA RC CHONGOLO SONGWE
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ndugu *Fadhili Maganya* amewasili katika mkoa wa Songwe rasmi kwa ajili ya kuanza ziara yake na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Daniel Chongoloambaye amemweleza namna ilani ilivyotekelezwa kwa vitendo.
Chongolo amesema kuwa ndani ya miaka minne ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan madarakani mkoa umeimarika kimaendeleo na kiuchumi huku akimuahidi zawadi ya kura za ushindi kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu.
Baada ya kusaini kitabu cha wageni, Maganya alimshukuru Chongolo kwa mapokezi mazuri aliyompa wakati alipowasili katika ofisi yake.



Maoni
Chapisha Maoni