RC MAKALLA AWAPONGEZA WANANCHI KWA KUYAKATAA MAANDAMANO YA DISEMBA 09


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Jumatano Disemba 10, 2025, amewapongeza wananchi kwa kuyakataa maandamano ya Disemba 09, 2025, akiwataka kujenga utamaduni wa kudumu wa kukataa maandamano na matukio yote yenye viashiria vya uvunjifu wa amani Mkoani Arusha.


Mhe. Makalla amebainisha hayo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za kibiashara kwenye soko la Kilombero Jijini Arusha, akiahidi kuwa serikali na Vyombo vya ulinzi na usalama Mkoani Arusha vitaendelea kuhakikisha usalama na amani inakuwepo.


"Dunia imeona na watanzania wameithibitishia dunia ya kwamba wakiamua kulinda amani wanailinda, wasiotutakia mema jana wameaibika. Watanzania wanapenda amani na hawajazoea mambo ya maandamano na uvunjifu wa amani na wale wote waliokuwa wanataka vurugu leo wamejifungua- wana maumivu kwani hawakufanikiwa." Amesema Mhe. Makalla.



Mhe. Makalla kadhalika kando ya kuwahakikishia wananchi ulinzi na usalama muda wote, amehimiza pia umuhimu wa wananchi kujikita katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii, akionya na kutangaza utimamu wa Vyombo vya ulinzi na usalama katika kukabiliana na wote wanaopanga kufanya vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani katika Mkoa wa Arusha.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE