RC MAKALLA AWAHAKIKISHIA USALAMA WANANCHI WA ARUSHA


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amewahakikishia usalama na utulivu wananchi wa Mkoa wa Arusha, akiwataka kuendelea na shughuli zao na kusema Vyombo vya ulinzi na usalama vipo tayari muda wote kuwalinda wao na mali zao.


Mhe. Makalla amebainisha hayo leo Jumatatu Disemba 08, 2025, wakati akizungumza na wananchi wanaoishi kwenye Mpaka wa Namanga, Wilayani Longido, unaounganisha Tanzania na Kenya, mara baada ya Kikao cha ujirani mwema cha Kamati za usalama za Mikoa ya Arusha na Rift Valley ya nchini Kenya.


"Nipo hapa kuwahakikishia Serikali na Vyombo vyote vya ulinzi na usalama vipo tayari kuwalinda Watanzania na mali zao zote na kwa maana hiyo kesho wana Arusha endeleeni na kazi zenu kama kawaida. Ni mapumziko lakini kazi za kiuchumi ziendelee kama kawaida kwani marufuku iliyopigwa ni ya maandamano." Amesema Mhe. Makalla



Akisisitiza wajibu wa serikali katika kulinda raia na mali zao, Mhe. Makalla pia amewahimiza Wananchi wanaoishi kwenye eneo hilo la mpaka kutoka Kenya na Tanzania kuwa mabalozi wa amani kwa kulinda amani na kutoa taarifa za matukio ya uvunjifu wa amani katika mpaka huo muhimu kwa uchumi wa Tanzania pamoja na Kenya.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE