WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE JIJINI ARUSHA


Imeelezwa kuwa zaidi ya 60% ya wafanyakazi wa moja kwa moja kwenye sekta ya utalii ni wanawake licha ya kukabiliwa na changamoto lukuki kwenye sekta hiyo inayochangia zaidi ya 17% ya pato la Taifa.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la wanawake jijini Arusha kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax amesema watahakikisha wanawake wananufaika zaidi na fursa zilizopo kwenye sekta hiyo.


Kwa upande wake naibu waziri wa maendeleo ya jamii jinsia wanawakena makundi maalum Mwananidi Ali Khamis anasema Rais Samia ameshafungua milango ya watalii hivyo wanawake wa Arusha na mikoa mingine wachangamkie fursa hiyo.

Dkt. Bakari George, Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) ambacho kina kituo cha utafiti na uhifadhi wa machapisho ya wanawake anasema Rais Samia hajahamasisha wanawake tu kwenye maswala ya uongozi bali hata wanaume.


Kongamano hilo la wanawake limebebwa na kaulimbiu isemayo ushiriki wa wanawake katika utalii na athari za ukatili wa kijinsia katika miaka 30 ya Beijing.






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE