MSOMERA WAFIKIWA NA ELIMU YA UNENEPESHAJI MIFUGO KUPATA MAZAO BORA YA NYAMA.
Katika kuhakikisha bodi ya Nyama Tanzania (TMB) inazifikia jamii hususani zile za kifugaji imeendelea kutoa elimu ya ufugaji bora katika kunenepesha mifugo ili kupata mazao bora ya nyama Mkoani Tanga katika Wilaya ya Handen Kijiji cha Msomera.
Akitoa elimu afisa Mifugo Festo Nzalallila amewaomba wafugaji kufuata taratibu za ufugaji na malisho sahihi ya mifugo yao ili kupata mazao mazuri ya nyama ambapo amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo kutaongeza soko la biashara hiyo ya mazoa ya nyama ndani na nje ya nchi.
Aidha afisa huyo wa mifugo amewambia wananchi wa msomera kuwa eneo hilo kwa ufugaji na malisho ni zuri hivyo anaimani mazao ya nyama yatakuwa bora na kuwafutia walaji wa nyama kutoka Msomera.
Vilevile amewasisitiza wafugaji hao kuwa ni vyema wakafanya ufugaji wa kisasa ambao matokeo yake ni mazuri kibiashara husu akigusia suala la unenepeshaji wa mifugo ili kupata mazao bora ya nyama.




Maoni
Chapisha Maoni