KUELEKEA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE KIMATAIFA; DCEA YASHIRIKI KUTOA ELIMU KINGA MADHARA DAWA ZA KULEVYA


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 04.03.2025 inaungana na Watanzania, Taasisi za umma na Sekta binafsi katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Kimataifa kwa kutoa elimu kwa jamii juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya katika viwanja vya TBA vilivyopo Kaloleni jijini Arusha. 


Machi 08, 2025 itakuwa ni kilele cha Maadhimisho hayo na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni; *Wanawake na Wasichana 2025:* *_Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji_*.


Wananchi waliofika katika banda la Mamlaka walipata fursa ya kuona aina za sampuli mbalimbali za dawa za kulevya lakini pia waliaswa kutowanyanyapaa waraibu wa dawa za kulevya wakiwemo waraibu wanawake kwani uraibu ni ugonjwa na unatibika. 


Wananchi waliofika katika banda la Mamlaka waliombwa kushirikiana na Mamlaka kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kupitia Kituo cha Miito ya Simu cha Mamlaka kwa kupiga simu ya bure 119.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE