DCEA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KIMATAIFA JIJINI ARUSHA

 


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 08.03.2025 inaungana na Watanzania, Taasisi za umma na Sekta binafsi katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Kimataifa kwa kutoa elimu kwa jamii juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya katika viwanja vya TBA vilivyopo Kaloleni jijini Arusha. 


Mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alihutubia umma katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni; *Wanawake na Wasichana 2025:* *_Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji_*.

Wananchi waliofika katika banda la Mamlaka walipata fursa ya kuona aina za sampuli mbalimbali za dawa za kulevya lakini pia kuona bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na waraibu waliopata nafuu kamavile sabuni na mikate.  

*_Wananchi waliofika katika banda la Mamlaka waliombwa kushirikiana na Mamlaka kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kupitia Kituo cha Miito ya Simu cha Mamlaka kwa kupiga simu ya bure 119_*.





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE