MSTAHIKI MEYA AZINDUA MAONESHO YA BODI YA MIKOPO (HESLB) KANDA YA KASKAZINI.


Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe.Maxmillian Iranqhe amezindua maonesho ya Bodi ya Mikopo(HESLB) kanda ya Kaskazini ambayo makao yake makuu ni Jijini Arusha. Mhe.Iranqhe ameongoza zoezi hilo akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mhe. Paul Makonda.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mhe. Iranqe ameipongeza bodi hiyo ya mikopo kwa kutimiza miaka 20 toka ianzishwe.

Mhe. Iranqhe amesema bodi ya mikopo imetimiza miaka 20 huku ikiwa imeisaidia jamii ya Watanzania wengi maskini kwa kupata elimu ya juu,imeongeza idadi ya wasomi nchini na wataalamu wa fani mbalimbali ambapo tangu kuanzishwa kwake hadi kufikia mwaka huu wa masomo wa 2024/2025 ,bodi hii imewezesha takribani Wanufaika zaidi ya laki nane kupata elimu katika ngazi ya vyuo vikuu na vyuo vya kati.


Aidha,bodi imeboresha mifumo yake yenyewe ya utoaji na urejeshaji wa mikopo ya wanafunzi kutoka kutumia nakala ngumu kuomba mkopo hadi sasa kutumia njia ya mfumo(online system)kuomba mkopo,kupanga mikopo na kurejesha mikopo hiyo.

Mhe. Mstahiki Meya amebainisha kuwa bodi ya mikopo imepiga hatua zaidi kwani kwa sasa inafanya kazi zake kwa kutumia mifumo(paperless) kwa takribani asilimia 95,ambapo kuomba likizo na masuala mengine yote ya kitumishi yamewekwa kwenye  mifumo.

Kwa upande wake Meneja wa Bodi ya mikopo kanda ya Kaskazini Bi. Lucy Kirigha amemshukuru Mstahiki Meya kwa kufika kwake kuzindua maonesho hayo na kutoa wito kwa Watanzania wenye sifa za kupata mikopo kutosita kuomba mkopo pindi dirisha la kuomba litakapofunguliwa.


Maonesho hayo yamehudhuriwa na kudhaminiwa na taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na NMB Benki,CRDB Benki,Tengeru Institute of Community Development,Arusha Technical college,NHIF,Chuo kikuu cha SAUT,Chuo kikuu cha Nelson Mandela,Chuo cha Madini,MWECAU,TANAPA,Chuo kikuu cha Arusha,Chuo kikuu cha Tumaini na UTT-AMIS.





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE