DCEA YATOA ELIMU KINGA KWA MTANDAO WA WASANII WA MUZIKI JIJINI ARUSHA


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 08.02.2025 imetoa elimu kinga juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya kwa wasanii wa muziki zaidi ya 30 walioshiriki Mkutano wa Mtandao wa Wasanii wa Mkoa wa Arusha katika Ukumbi wa Metropole Cinema Hall uliopo jijini Arusha. 


Mgeni rasmi wa mkutano huo alikuwa ni Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maxmilian Iranghe. Wasanii hao walihimizwa waache kujihusisha na dawa za kulevya sababu vitendo hivyo vinaweza kuwakatishia ndoto zao za kimuziki hadi kufikia kufungwa jela miaka 30 au maisha. 


Pia walihamasishwa kutoa nyimbo ambazo zina ujumbe wa kupiga vita dawa za kulevya na kuhamasisha jamii watoe taarifa za wahalifu kupitia namba ya simu ya bure ya 119. Hivyo wasitoe nyimbo zinazohamasisha tatizo hilo sababu wao ni vioo vya jamii, baadhi ya watu wanaweza kuiga. 





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE