DCEA YAHITIMISHA ZIARA YA UTOAJI ELIMU KINGA KWA WANAFUNZI MKOANI KILIMANJARO
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini tarehe 12.02.2025 imetoa elimu kinga kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mawenzi na Shule za Msingi Mwenge, Uhuru, Mawenzi na Rau juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya mkoani Kilimanjaro.
Jumla ya wanafunzi zaidi ya 1500 walipatiwa elimu kinga. Pia ilitembelea nyumba za upataji nafuu ambazo ni Kilimanjaro New Vision Sober House, Kilimanjaro New Vision Women Sober House na Kilimanjaro Recovery Center Sober House ikiwa na lengo la kufuatilia maendeleo ya waraibu wanaoishi nyumba hizo na pia kuangalia kama wanatekeleza kile kilichoelezwa kwenye miongozo ya nyumba za upataji nafuu.
DCEA Kanda ya Kaskazini itaendelea kuzitembelea nyumba za upataji nafuu ili kubaini changamoto wanazopitia na kuzitafutia suluhisho ili waraibu wapate huduma za matibabu sahihi kwenye nyumba hizo.




Maoni
Chapisha Maoni