WADAU PAMOJA NA REA WAUNGA MKONO KAMPENI YA NISHATI SAFI

 


Wakala wa nishati Vijijini ( REA )kwa kushirikiana na wadau wa tekinolojia mbalimbali za nishati safi wamuunga mkono Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kuhakikisha ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia. 


Ikumbukwe kwamba hivi karibuni mei 8 Mwaka huu 2024 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere ( JNICC ) jijini Dar es salaam,Rais wa jamhuri ya Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan alizindua Mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia na kukawa na maelekezo aliyoyatoa ili kufuatwa na kuzingatiwa ikiwa ni pamoja na mkakati wa ushikiano wa pamoja Serikali na sekta binafsi katika utekelezaji ili kufikia lengo hilo lililoanza mchakato wake tangu mwezi November mwaka 2022.


Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya saba (7) ya tekinolojia ya madini viwanja vya Bomba mbili Geita Kaimu Meneja wa usaidizi wa kiufundi kwa uendelezaji wa miradi wakala wa nishati vijijini (REA).Mhandisi Emmanuel Yesaya amesema wameitikia wito wa kauli mbiu ya utekelezaji huo isemayo ( 'Matumizi ya Teknolojia sahihi na nishati safi katika Sekta ya Madini kwa maendeleo endelevu") na kumuunga Mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji huo na matarajio ya ujio wa Rais katika maonyesho hayo ili kutoa Elimu na fursa mbalimbali ambazo REA unazitekeleza katika kuunga mkono sekta ya madini na matumizi ya nishati safi.


Mhandisi Yesaya amesema na katika kuunga mkono nishati safi ya kupikia Wakala wa nishati vijijini - REA wameleta majiko ya LPG ya kilo sita 6 ambayo yanauzwa kwa bei ya Ruzuku mpaka asilimia 50.


Amesema serikali imeweka punguzo la asilimia hamsini (50) hiyo ili kuwawezesha wananchi watanzania kuweza kumudu gharama hiyo nafuu ya manunuzi ya majiko hayo ya LPG.


Amesema kutoka kwenye bei halisi ya mtaani majiko yanayouzwa kiasi cha shilingi Elfu thelasini na tano (35) kwa ule mtungi wa kilo sita 6,ndani ya banda la REA katika maonyesho hayo yanapatikana kwa bei nafuu kwa kulipia kiasi cha shilingi elfu kumi na saba na miatano tu (17,500/=) pale utakapo enda ukiwa na kitambulisho cha Taifa yaani kitambulisho cha (NIDA).


Amesema lengo la mnunuzi wa Jiko hilo kwenda na kitambulisho hicho ili kusaidia kusajili taarifa za mnunuzi lango ni kuwa Mtanzania aweze kupata jiko la gesi ili aweze kutumia nishati safi ya kupikia.


Mhandisi Yesaya ametoa wito na ombi kwa wananchi wa Mkoa wa Geita na mikoa jirani na watu wote kwa ujumla wanaoweza kujitokeza kushiriki kwenye maonesho hayo wajitokeze kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo ya ununuzi wa majiko hayo ya nishati safi ya gesi kwa bei nafuu ya Ruzuku iliyowekwa na serikali yetu na kwenda kuyatumia.


Kwa kufanya hivyo ni kumuunga mkono Rais wetu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan katika kampeni yake ya kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2034,sawa na miaka kumi 10 ijayo asilimia 80 ya watanzania watakuwa wanatumia nishati safi ya kupikia.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE