KIRUSWA AIPA KONGOLE BOT


NAIBU wa waziri wa Madini  Dkt.Steven Kiruswa  ameipongeza Benki kuu ya Tanzania (BOT) Kwa  kazi nzuri wanayofanya kwa kuendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wa madini na wadau mbalimbali kwenye sekta ya madini 

Dkt Kiruswa ameyasema haya leo Oktoba 12, 2024 mara baada ya kutembelea kwenye banda la Benki kuu katika viwanja vya maonesho bombambili mkoani Geita .

 kwa upande wake Sajent Rebecca  Manase Afisa wa Jeshi la polisi kituo cha polis Geita akizungumzia huduma zinazotolewa na benki hiyo  amesema amepata fursa ya kutembelea banda la Benki kuu ya Tanzania (BOT) kwenye maonyesho ya saba ya tekinolojia ya madini na ameweza kujifunza mambo mengi yenye faida na ya msingi.

Sajeti  Rebecca amesema kuwa ametembelea kuona namna benki kuu wanavyofanya kazi lakini pia kujua juu ya matumizi ya noti na kuweza kuitambua noti ambayo haitumiki kiserikali.

"Nimeweza kufahamu zaidi juu ya matumizi ya noti na wananchi namna wanavyoweza kufaidika na benki kuu  na kutambua noti ambayo haitumiki "amesema Sajeti Rebecca

Ameongeza kuwa amepata  elimu ya kutosha kutoka benki kuu hivyo amewaasa wananchi kutembelea banda hilo ili waweze kupata elimu.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WAGOMBEA,WANACHAMA WA CCM VILIO JUU YA KURA ZA MAONI HAI

BARAZA LA ARDHI LAFUTA KESI YA ARDHI KUTOKANA NA DOSARI ZA KISHERIA

TAWIRI YAWAKARIBISHA WADAU KUFANYA TAFITI KATIKA SPISHI MUHIMU YA SOKWE